Mambo Jambo
JF-Expert Member
- Jul 11, 2008
- 1,100
- 82
Jana katika kituo cha Television cha DTV kulikuwa na mahojiano kati ya waandishi wa habari wa kituo hicho na Waziri wa habari, utamaduni na michezo, George H. Mkuchika, waandishi hao walipata fursa ya kumuuliza Mh Mkuchika maswali mengi yakiwemo ya habari, utamaduni na michezo.
Baadaye mwandishi wa DTV alitaka kujua msimamo wa Mh Mkuchika kuhusu hali ya sasa ya chama cha Mapinduzi CCM akiwa kama Naibu katibu mkuu wa chama hicho, mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo:-
Mwandishi wa DTV:- Mh Mkuchika ukiwa kama waziri mwenye dhamana ya wizara ya habari,utamaduni na michezo na vilevile ukiwa kama Naibu katibu mkuu wa chama cha mapinduzi CCM ningependa kuuliza swali. Hivi sasa chama chenu kimepoteza imani kwa wananchi na vile vile kunaonekana wazi kuwa na kambi mbili ndani ya chama chenu kimoja na hii inazidi kudhihirika kila siku kutokana na wanachama na viongozi wa chama hicho kuendesha mikutano ya waandishi wa habari na kuelezea mambo mengi yenye kukinzana na kuchafuana, Je, wewe kama kiongozi wa serikali na Naibu katibu mkuu wa CCM unasema nini kuhusu hili?
Mkuchika: Ni kweli kumekuwa na malumbano mengi kwa baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM lakini hiyo haipunguzi imani ya wananchi kwa CCM watu kuwa chama kimoja haina maana kuwa watakuwa wanakubaliana na kila jambo, lakini jambo la msingi ni kwamba watu hawa wanaoitisha mikutano na waandishi wa habari majumbani kwao, kwenye vilabu, maelezo ndiyo wanaosababisha yote haya ndiyo wanaofanya chama kionekane kinayumba, mambo ya chama yanabidi yaongelewe ndani ya vikao vya chama na siyo kila mmjoja akijisikia kuita waandishi wa habari na kuongea anachojisikia hayo ni makosa makubwa na ninaongea hayo nikiwa kama kiongozi wa chama na mwenye dhamana kama kiongozi ndani ya CCM.
Mwandishi wa DTV: Sasa hauoni mambo kama haya yanaweza kuzidi kupunguza umaarufu wa chama chenu cha CCM?
Mkuchika: Vitu hivi vinavyoendelea hivi sasa kamwe havitapunguza umaarufu wa CCM bali vitapunguza umaarufu wa hao wanaoitisha mikutano na waandishi wa habari kila siku na kuongea mambo ambayo kiutaratibu inabidi yamalizwe ndani ya chama.
Baada ya hapo niliendelea na shughuli zangu hakukuwa na mpya.
NOTE: Niliyoandika siyo mstari kwa mstari kama mahojiano yalivyokuwa lakini kwa kifupi ndiyo hivyo, labda kama kuna mtu anayeweza kuyapata hayo mazungumzo on tape ayamwage hapa.
MJ