Ila umesikia au kusoma mchezaji katika nchi hizo anazima simu ili viongozi wasimpate?Kama mchezaji una haki ya kukataa kusaini ili kupata maslahi zaidi au kuondoka hiyo ni haki yako ya kimsingi. Ila huwezi kusikia mchezaji mkataba haujaisha anasema naenda timu fulani. Kwa sababu Tanzania sheria zinazotawala mpira hazifuatwi ndio unaona viongozi na wachezaji wanafanya wanavyotaka .Mchezaji yupo kwenye mkataba haheshimu mkataba .Anajua wazi kwamba uamuzi wa suala lake utapigwa danadana. Mfano suala la Kessy,Simba waliambiwa walete risiti za mshahara wake wa miezi 3 ya mwisho wa mkataba.Wamepeleka hakuna uamuzi.Utasikia kutaneni muamuwe wenyewe.Mohamed Mkopi amesign Mbeya Stars huyu akiwa na mkataba na Prisons kafungiwa mwaka 1.Hamna cha kutaneni mpate muafaka. Sheria zifuatwe viongozi na wachezaji itabidi nao wafuate sheria watakapoona hamna longolongo.Duu kweli bongo tuna safari ndefu sana. Sijawahi kusoma au kusikia kiongozi wa timu zilizoendelea huko ulaya, Amerika na kwingineko kiongozi akitoa komenti kama hizo. Eti 'mchezaji mwenyewe hata asipokuwepo kwenye timu madhara hayaonekani' Sasa kwa nini bado wanamchezaji ambaye ni mzigo!? Mimi nashabikia Yanga lakini km ni kweli Hans amesema hivyo amenisikitisha. It's unprofessional!!
Sikukumbuka ndio nimekumbuka saiziUlikumbuka kuidharau ilipomchukua Tambwe na Yondani...?
Ndio viongozi wa soka wa kibongo haoDuu kweli bongo tuna safari ndefu sana. Sijawahi kusoma au kusikia kiongozi wa timu zilizoendelea huko ulaya, Amerika na kwingineko kiongozi akitoa komenti kama hizo. Eti 'mchezaji mwenyewe hata asipokuwepo kwenye timu madhara hayaonekani' Sasa kwa nini bado wanamchezaji ambaye ni mzigo!? Mimi nashabikia Yanga lakini km ni kweli Hans amesema hivyo amenisikitisha. It's unprofessional!!
Simba imeishakuwa feeder club!Sio mbaya akienda, yanga naona inakuwa simba B sasa kuanzia kwa Barthez, kessy, mkude na tambwe, hapo tayari idara zote covered. Kipa, beki, kiungo na straika.
Viongozi wa mpira bongo bwana-'Eti kwa vile Mkude ni mchezaji ambaye tumemkuza wenyewe na tumekabidhi majuku, lakini anajifanya amekuwa na wakati hata asipokuwepo kwenye timu hatupati madhara yoyote,”amesema Hans Poppe.19:27LIGI KUU BARA
Shaffihdauda
Kudai haki yake ya msingi kumesababisha mchango wake ndani ya timu kutothaminika na kutishiwa kutemwa mwishoni mwa msimu huu
Klabu ya Simba ipo kwenye mpango wa kusajili mbadala wa nahodha wao Jonas Mkude, baada ya mchezaji huyo kugoma kusaini mkataba mpya huku akiutolea maneno ya hovyo viongozi wake.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Zacharia Hans Poppe ameiambia Goal, wamechoshwa na maneno ya mchezaji huyo na sasa wanaona nivyema wakamtafuta mchezaji mwingine ambaye atamudu kwenye nafasi hiyo.
“Tumeanza mipango ya kutafuta mchezaji mwenye uwezo zaidi ya Mkude, wa nafasi ya kiungo mkabaji kwasababu mchezaji huyo amekuwa na maneno mengi kuliko mchango wake kwenye timu,”amesema Hans Poppe.
Kiongozi huyo amesema mchezaji Mkude anataka kupewa dau kubwa kama ilivyo kwa wachezaji wa kimataifa, lakini kiwango chake ni chakawaida hivyo wanaona nivyema wafanye maamuzi mapema katika kipindi hiki cha dirisha dogo.
Amesema hadi sasa hakuna mchezaji waliyemlenga lakini wamepanga kumtafuta mchezaji huyo kwenye mataifa ya nje kwakua wanataka mtu mwenye uwezo tofauti kwa ajili ya kuifikisha mbali timu yao hasa ukizingatia wanamatarajio ya kupata nafasi ya kucheza michuano ya kimataifa siku zijazo.
“Mkude ni mchezaji ambaye tumemkuza wenyewe na tumekabidhi majuku, lakini anajifanya amekuwa na wakati hata asipokuwepo kwenye timu hatupati madhara yoyote,”amesema Hans Poppe.
Yanga yamtema rasmi Mbuyu Twite
Katika siku za karibuni Mkude, aligoma kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea Simb, baada ya viongozi wa timu hiyo kumpa kiasi kidogo cha pesa na yeye kutaka kupewa dau la milioni 80 badala ya 50 wanazotaka wao.
Baada ya uongozi kugoma kutoa kiasi hicho cha pesa Mkude amesema ataondoka na kujiunga na mahasimu wao Yanga baada ya mkataba wake kuisha mwishoni mwa msimu huu.
Mkude amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Simba, na amecheza mechi zote za mzunguko wa kwanza wa ligi ya Vodacom Tanzania na kuifaya timu hiyo kumaliza nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 35.
View attachment 442508
Jibu muafaka kabisa. Simba sasa ni feeder club. Inatengeneza wachezaji ili waende club kubwa. Hilo sasa halina mjadala.Mkuu naomba tu nikusaidie.!
Simba SC ndio academy ya Yanga..! Kwa kuwa wachezaji wanatoka simba kwenda Yanga kuishi ndoto zao....za Mafanikio...
Umeona wapi Kikosi cha pili cha Barca kikawa kinashinda Ubingwa wakati kikosi cha kwanza hakijatwaa ubingwa kwa miaka 5?
Soma kwanza uelewe kilichoandikwa!Mpira wa Barcelona unaangaliaga chooni au?
Mkude anataka walau passport yake igongwe muhuri. Toka aipate haijawahi gongwa muhuri!Sio mbaya akienda, yanga naona inakuwa simba B sasa kuanzia kwa Barthez, kessy, mkude na tambwe, hapo tayari idara zote covered. Kipa, beki, kiungo na straika.
Endeleeni kujisifia kuwa makini kusajili viungo ikiwa Safu ya Ushambulizi na Ulinzi iko hoi...Ndiyo ujinga wa kukuza vitimu vya watoto klabuni,, unahangaika kuvihudumia kwa muda mrefu na kurisk ktk mechi muhimu kwa kuvipa nafasi ili vicheze na kupata uzoefu baadaye wakisha pata uzoefu wanaanza maneno Mbofu mbofu.
Aende tu Yanga akacheze huko pale atakuja mwingine Simba haijahi kufanya makosa ktk usajili wa kiungo toka Enzi za Nico Njohole,, Gaga,, Renny ,, Michael Paul nk.
Yanga iachane na huyo mamluki wa Simba