Mkude sasa uhakika first 11 ya Simba

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253

Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog amesema kuwa kitendo cha kiungo wake, Jonas Mkude cha kuonyesha kiwango cha juu katika mechi Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga, sasa anaweza kumuanzisha katika mchezo wa Jumapili dhidi ya Mbeya City.

Endapo, Mkude atafanikiwa kuanza katika mechi ijayo basi hiyo itakuwa ni mara yake ya tatu kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo tangu kuanza kwa msimu huu.

Mechi ya kwanza kuanza katika kikosi cha kwanza msimu huu ilikuwa ni dhidi ya Mwadui FC kisha Mtibwa Sugar. Michezo mingine yote aliyocheza alikuwa akianzia benchi.

Omog alisema kutokana na uwezo ambao Mkude amekuwa akiuonyesha kila anapoingia uwanjani hususan dhidi ya Yanga bila shaka anaweza kumwanzisha dhidi Mbeya City, siku ya Jumapili.
“Mkude hivi sasa yupo vizuri na amekuwa akionyesha kiwango cha juu kila mechi anayocheza, hata hivyo kuna vitu nimevibaini kwa hiyo naweza kumwanzisha katika mechi yetu na Mbeya City,” alisema Omog.

Simba itapambana na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, mchezo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani Mkubwa.

SOURCE: CHAMPIONI
 
Yule Kocha Boya sana

ameona jahazi linazama ndio anamkumbuka Mkude

Tangu mechi ya ngao ya hisani gape la mkude lilionekena

Mechi ya mbao ndio lilikuwa wazi zaidi

Ya juzi ya yanga ndio huyo alirudisha uhai wa timu

sasa kocha alikuwa haoni hayo yote
 
Omog barua yake ipo tayari inasubir tu apoteze mchezo isainiwe ipigwe mhuri atambae
 
hakukuwa na haja ya ya ya kuleta rundo la wachezaji msimu huu kwan kikosi cha mwaka jana kilikua kizuri mno kilihitaji kuongezewa nguvu kdg tu.....manula na okwi tu ndo waliotakiwa kuongezwa huyu mwangne ananogesha jukwaa tu but mchango wake kwe timu kupata matokeo ni mdg mno, simba imetumia miaka mitatu iliopita kujenga timu kutoka kwa vijana wadogo na ilikua imefikia pazuri sana lakini ajabu timu ikaona heri ajibu aondoke lakin eti tumlete niyonzima kweli?
 
Siamini kama mkude anaweza kumweka nje James Kotei kwa sasa labda kama kunashinikizo au Kotei awe mgonjwa. Kotei anasifa za kuzuia na kushambulia tena kwa kasi, Pasi zake ni za mmoja kwa moja, anapenda kuongeza mashambulizi dhidi ya Timu pinzani wakati mkude ni kiungo wa kuzuia, anapenda kupiga Pasi sana tena za pembeni zisizo na madhara kwa timu pinzani. Mkude yupo tararibu ila ana faasana kamatimu imeshinda ili akae na mpira timu iwe inapoteza muda.
 
Hata Nyoni na Mbonde walihitajika sana kwa ajili ya kupanua kikosi.
 
Wanaweza hata kutumika pamoja kama Coach akiwagawia majukumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…