Mkufunzi atoa hadhari kwa wamama wanaonyonyesha wale waliozidi uzito

Mkufunzi atoa hadhari kwa wamama wanaonyonyesha wale waliozidi uzito

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mkufunzi wa Mazoezi kutoka Shirika la Vyama vya Magonjwa Yasiyoambukiza (NCD), Dk. Waziri Ndonde amesema katika kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza kwa mwanamke anayenyonyesha mwenye uzito kupita kiasi, anatakiwa kutumia dakika 150 kwa wiki kufanya mazoezi.

Dkt. Ndonde alitoa angalizo hilo jana wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza kilichofanyika mkoani Mwanza na kudhuriwa na watu mbalimbali.

Alisema dhana kubwa ya kujikinga na kuzuia magonjwa hayo ni pamoja na kuzingatia masuala ya lishe, kutokutumia tumbaku na kuushughulisha mwili kwa kufanya mazoezi.

"Kuushughulisha mwili na kufanya mazoezi ni kitu cha msingi cha kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza, pamoja na lishe, ukiwa na tabia bwete, kuishi bila kuushughulisha mwili ni moja ya sababu ya kupata magonjwa haya," alisema.

Mtaalamu huyo alisema serikali katika kutambua hilo, mwaka jana kwenye wiki kama hiyo, Wizara ya Afya ilizindua mwongozo wa kushughulisha mwili na kufanya mazoezi katika kuepuka tabia bwete.

"Mwongozo huu tayari umeshachapishwa na wadau mbalimbali wamepewa wanaendelea kupata elimu, moja ya lengo kubwa la wiki hii kwa mwaka huu ambapo tunaadhimisha hapa Mwanza, ni kuelimisha watu zaidi mapendekezo ambayo yapo ndani ya mwongozo huo," alisema

Aliongeza kuwa mwongozo upo wazi kwa watu wa rika zote, mfano wenye magonjwa sugu na wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU), umeelekeza namna gani ya kuushughulisha mwili kwa kufanya mazoezi.

Pia alisema kulikuwa na shida nyingi kwa wajawazito na waliojifungua, zinazotokana na mila na desturi wanakuwa na uzito uliokithiri baada ya kujifungua kutokana na lishe wanayopewa.

"Mwongozo unamtaka huyu mama atumie angalau dakika 150 kwa wiki wakati anatunzwa kupewa chakula bora ili apate maziwa ya kumnyonyesha mtoto, dakika hizo azitumie kwa wiki kuhakikisha hatapata unene uliokithiri, dakika hizo atatakiwa kufanya mazoezi yote muhimu," alisema.

Pia alisema mwongozo huo umetoa maelekezo kwa wazee, yaani watu wenye umri wa zaidi ya miaka 65, kuhusu nini wanapaswa kufanya ili kuepuka magonjwa hayo.


Chanzo: IPP
 
Mkufunzi wa Mazoezi kutoka Shirika la Vyama vya Magonjwa Yasiyoambukiza (NCD), Dk. Waziri Ndonde amesema katika kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza kwa mwanamke anayenyonyesha mwenye uzito kupita kiasi, anatakiwa kutumia


Chanzo: IPP
Kwa nyongeza naomba niseme kuwa

Dakika 150 ni sawa na Masaa mawili na nusu.
 
Back
Top Bottom