Binti Mzalendo
Member
- Aug 3, 2022
- 27
- 18
Aliesema kilimo ni uti wa mgongo wa taifa hakukosea,lakini ni uti wa mgongo kwa wajanja wenye pesa na SI mtu wa Hali ya chini.
Kilimo ni sayansi ya uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.Mkulima anapoandaa shamba,anapanda,anapalilia mategemeo yake ni kuvuna mazao Bora na hata ainuke kimaisha.lakini kwa mkulima mdogo hii imekuwa changamoto sana.
Kilimo ni sayansi ya uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.Mkulima anapoandaa shamba,anapanda,anapalilia mategemeo yake ni kuvuna mazao Bora na hata ainuke kimaisha.lakini kwa mkulima mdogo hii imekuwa changamoto sana.
Shida ni nini?, Nahisi umewahi kukutana na neno walanguzi wa mazao,hawa watu wapo wenye Nia njema na wale wajanja wajanja wanaopiga pesa kwa kumkandamiza mkulima tunawaita "makanjanja".Mkulima anapokomaza mazao shambani akiwa anavuna hawa walanguzi wajanja wajanja huja hadi shambani na kumlaghai mkulima kumuuzia mazao shambani kwa bei ya chini kabisa, ambapo angeifadhi angeuza kwa bei nzuri, sisemi kama wanalazimishwa sana lakini tunajua mchezo wa pesa hapo huna hata mia unaoneshwa laki utaingiwa na matamanio tu. Kama mnataka mazao na Mimi SI mkulima na nyie wafanyabiashara kwanini tusiuziane bei yenye manufaa kwa kila mmoja na kwanini umnyonye mkulima?.
Hapo mbegu yenyewe Serikali inatoa mbegu nzuri wajanja wanachakachua mkulima mdogo anaishia kuchukua mbegu ya kawaida na Bado anauza mazao kwa hasara,serikali iingilie kati Ili suala na wakulima.
Wapate elimu ya kutosha.
- Kuwe na sehemu husika ya wakulima kuuza mazao yao.
- kuwe na bei iliyopangwa yenye makubaliano na wakulima.
- Mbegu zitolewazo na Serikali ziwafikie wakulima wadogo wadogo.
- Wakulima watambue thamani yao na waache kuingiwa tamaa ya kuuzia mazao shambani.
Neno langu kwa hawa walanguzi wenye Nia Ovu,nyie ndio mnaoangusha Pato la taifa kwani mnashindwa kupanga bei ambayo haimuumizi mkulima? Bei ambayo hata wewe itakupa baraka ikuondoe kwenye dhuluma.
Serikali na viongozi Ili suala mliangalie kwa mara nyingine mkulima mdogo anaonewa na atabaki kuwa mdogo sababu ya hawa walanguzi.kalamu naweka chini.
Upvote
3