SoC01 Mkulima wa Jembe la Mkono Tanzania

SoC01 Mkulima wa Jembe la Mkono Tanzania

Stories of Change - 2021 Competition

Jimytz

Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
6
Reaction score
3
TEGEMEO LA MKULIMA WA JEMBE LA MKONO

Ni zama hizi hizi za karne ya 21 ambayo bado mkulima anatumia jembe la mkono katika kipande cha ardhi alichobakisha baada ya unyanganyi wa mabavu wa wawekezaji wakipewa nguvu na viongozi hawahawa tulio waamini na kuyaamini maneno yao,

Tuachane na hayo maana siasa ya sasa ukiongea sana ndo mwanzo wa kuiona lupango. kwa jembe la mkono lizalishe chakula cha kuikimu familia yenye uwezo mdogo inayopambana kumpeleka mtoto shule, shule ambayo haina hata walimu, haina vifaa vya ufundishiaji, mzingira mabovu ya kusomea na kufundishia,harafu atoke kiongozi na kusema shule za serikali hazifaulishi vizuri..zinafaulisha vipi, kwa mpango wa elimu bure? Elimu bure isiyokuwa na maktaba,maabara,walimu? Hakika inasikitisha.

Ni jembe hilohilo la mkono limuwezeshe mkulima kuuza mazao yake aliyolima na kuvuna kwa nguvu nyingi na jasho, huku wahenga wakisema mchumia juani hulia kivulini, lakini mkulima huyu wa kijiji fulani hapa hapa Tanzania asiyethaminika anachumia juani na bado analia juani, 2 kwani masoko ya kuuza mihogo, kuuza karanga, kuuza nyanya na vitunguu yametawaliwa na washikadau wanaojipangia bei wazitakazo, bei inayomuacha mkulima akisononeka na viganja vilivyo jaa sugu za jembe na miguu iliyojaa kovu na alama miiba miguuni,

Mkulima huyu huyu anapiga moyo konde na kukipokea hicho kidogo angalau anunu mkate kwa ajili ya familia yake inayoyomtegemea Mkulima huyu huyu aliyekipokea kidogo hata kisichohifadhika benki wala mtandao wa simu kwa ajili ya akiba anarudi nyumbani akiwa ameinamisha kichwa, na hapo tayari kashakatwa tozo(kodi)kwa kumtumia mwanae aliye shule ya upili ili alipie pesa ya uji, uji usiokua na sukari wala kitafunio unamfanya mwanafunzi asinzie darasani baada ya kuuweka kinywani mwake

Uko wapi ufauruji wa huyu mtoto wa mkulima ambaye mwisho wa muhula atapambanishwa na mtoto wa kigogo Fulani aliyempeleka mtoto wake international school kwa kutumia pesa ya tozo kutoka kwa mkulima. “Kilimo ni uti wa mgongo”ni maneno ya wahenga, na ni maneno tunayo aminishwa katika maisha ya kila siku kupitia Makala mbalimbali bila kujua kwamba ni msemo tu amabao hata hauna ukweli ndani yake, mkulima wa kijijini kwetu huwezi kumuaminisha usemi huu kwani uti wa mgongo wake haujainuliwa na hiki kilimo cha jembe la mkono.

Tanzania ni nchi iliyochukua uhuru kutoka kwenye mikono ya Waingereza baada ya kazi kubwa iliyofanywa na wazalendo wakiongozwa na hayati Mwl. J.K Nyerere na mwaka 1961 Tanzania ilijipatia uhuru wake. Kiongozi huyu aliamini sana katika kilimo lakini sio hiki cha mkono,sio kilimo cha jembe, ni pale aliposikika akisema”Tubadili kilimo chetu kwa sababu kilimo kitusukume, kwa sababu hakuna kitu kingine cha kutusukuma nchi hii isipokuwa kilimo.

Lakini hichi kilimo hichi cha kutegemea mvua, kilimo hiki hakinambolea, hakina dawa, hakina maarifa, unalima harafu unapanda ovyo ovyo tu. Hakitusaidii sana hiki” Yalikua maono ya kiongozi aliyeangalia mbele sana, lakini bado,bado toka atoweke hadi sasa maneno yake hayajafanyiwa kazi ipasavyo, sasa utajiuliza kwamba, uwezo wa kuyazingatia aliyoyasema na kufata kilimo cha kisasa hakuna au uwezo upo lakini huo uwezo unaishia kwa wachache? Sina majibu pia.

3 Tangu wakoloni watuletee teknolojia ya mashine mnamo karne ya 18, kukawepo mashine rahisishi za kazi, ni kweli zimewasaidia na kuwainua wakulima baadhi katika nchi hiii, vipi kuhusu huyu mkulima mwingine asiyethaminika au labda yeye ana jina lake na sio jina la "MKULIMA?"La hasha! ndo hilo hilo jina lake, nilifikiri labda kwakua nchi yetu inayosifika kuwa na amani, upendo na maliasiri mbalimbali, pia ina watu wanaolipwa mamilioni ya pesa kila mwezi, basi ingejitahidi japo kuzigawa hizi mashine kwa hawa wakulima ili kuwainua na wao waweze kujiita "WAKULIMA" Nikafikiria tena labda pembejeo ndio kikwazo, kwanini wasigawiwe pembejeo wakulima hawa wanaoteseka na mbegu zenye kudumaa hata kabla ya mavuno.

Kama haitoshi mkulima huyuhuyu mpambanaji akaboreshewa barabara anayoitumia kufika mjini angalau basi kusiwe na gharama za kumuumiza anaposafirisha hicho kidogo alichokivuna. Kwakua ni mkulima hohe hahe kwanini hizi tozo zinazompunguzia alichokihangaikia kwa msimu mzima zisipunguzwe au kutolewa kabisa, ili kumfanya akawa huru na akalipa kodi nyingine stahiki nje na zile za miamala!! Inasikitisha sana, inasikitisha kwasababu ni mjumbe huyu huyu, mwenyekiti, diwani, mkuu wa wiliya, mkuu wa mkoa, mbunge, waziri na viongozi wakubwa wa nchi anategemea kutumia mazao kutoka sehemu mbali mbali za nchi hii ambayo yanazalishwa na mkulima wa jembe la mkono.

Maendeleo ya sayansi na teknolojia yako wapi sasa, ule mpango wa kuzisaidia kaya masikini uko wapi?? unamsaidia masikini kwa kumpatia pesa?la hasha huo sio msaada, huko ni kumfanya aendelee kuwa dhoofu na tegemezi kila iitwayo leo. Kama utayari wa kuzisaidia kaya masikini ambazo wingi wake ni wakulima wa jembe la mkono, basi wapatiwe mashine na penjeo, harafu tuwapatie rawama wao wakishindwa kujikwamua kutokana kwenye wimbi zito la umasikini.

Nchi ya Tanzania ina eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 945,087, maana kwamba ina ardhi ya kutosha, Ardhi inayotosha kwa kizazi cha leo chenye Zaidi ya watanzania milioni 60 na kijacho.4 Iweje leo baba au mama aliye rithishwa ardhi na mzazi wake , aliye ipokea hiyo ardhi kutoka kwa baba mzaa baba yake miaka lukuki iliyopita ipokonywe na kumilikishwa na watu wanaojiita wawekezaji??au ndo unapotumika msemo/ neon la kwenye kitabu kitakatifu (Marko 4:25) “kwa maana aliye na kitu ataongezwa, na asiye na kitu atanyang’anywa hata kile kidogo alichonacho” Japokua hili neon lipo katika kitabu kitakatifu lakini lisitumike kama lilivyoandikwa na kusomeka, tunawakosea sana hawa wamilikiji wa ardhi, ardhi zinazotegemewa kupaluliwa kwa jembe la mkono ila kupata chochote kitu.

Unamuacha na hali gani mkulima huyu? kwa hali hii ujitoe na kusema kuwa una mpango wa kupunguza kaya masikini??! utayatwanga maji kwenye kinu na matokeo yatakurukia na kukulowanisha mwenyewe, itabaki kuwa fedheha kwa nchi jirani unayojipambanisha nayo katika nyanja ya "UCHUMI" Mkulima na jembe, jembe na mkulima pole sana wewe mkulima unayelitegemea jembe kama mtaji wako, najua pole haitakusaidia lakini itakufariji na kukutia nguvu, endelea kuishi kwa mategemeo, ipo siku ipo siku, labda washuke maraika kutoka mbinguni ila sio kwa uwanda huu uliugubikwa na umimi.

Naipenda nchi yangu, naipenda Tanzania na mimi ni mtanzania mzalendo mwenye mtazamo chanya juu ya uendelezaji wa kilimo, ili kiukwamue uchumi wa mtanzania na Tanzania kwa ujumla. Naomba Makala hii iwafikie wakubwa wan chi hii, wajue kuna watu wanalia, sio kwamba hawawezi ila kuna watu wanasababisha wao washindwe. Kilimo ni uti wa mgongo, kilimo ni ajira, kilimo ni daraja la kuufikia uchumi

CROPED 1.jpg


croped.jpg
 
Upvote 1
Back
Top Bottom