Bundimwema
New Member
- Feb 26, 2024
- 1
- 0
“Nina Watoto nane, shughuli yangu kubwa ni Kilimo cha Mwani ambayo ni miongoni mwa mazao ninayoyategemea kunipatia mkate wa kila siku. Nafanyia shughuli zangu katika Kijiji cha Shamiani Kangani, Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba. Hapa ndipo pia ninapoishi.
Nimekuwa na ndoto ya kuwa mkulima bora na kupata manufaa kupitia Kilimo cha Mwani, lakini hiyo ndoto hadi sasa inasuasua. Sera ya Uchumi wa Buluu katika Kilimo cha Mwani, haitekelezwi kama ilivyopasa.” Hayo yamesemwa na Mkulima wa Mwani, aliyeko Zanzibar.
Kama ilivyo kwa Wakulima wengi wa mwani, Time Makame Shaali (47), hutumia zaidi ya saa 8 kila siku na TZS 18,000/- kwa wiki, katika maandalizi ya mashamba ya mwani. Mashamba hayo huhitaji kuwa na vifaa mbalimbali kama vile kamba, tai tai pamoja na pegi, ambazo hutumika katika kilimo cha mwani.

Pamoja na gharama zote hizo anazoingia Mkulima, uwezekano wa gharama hizo kurudi na kupata faida ni sawa na mchezo wa bahati nasibu. Hii ni kutokana na bei ya bidhaa hiyo, ambayo kwa sasa ni TZS 800/- kwa kilo.
Takwimu za Afisa Mdhamini Wizara ya Uchumi wa Buluu Dkt. Salim Mohammed Hamza, zinaonesha kuwa Wazanzibari 20,000 wanajishughulisha na Kilimo cha Mwani, ambapo asilimia 80 ni akina mama.
Kisiwa cha Pemba pekee, kina wakulima wa mwani wapatao 10,000 ambapo asilimia 90 ya wakulima hao, wanapatikana Mkoa wa Kusini Pemba, hasa ukanda wa Magharibi mwa Mkoa huo na asilimia 10 kutoka Mkoa wa Kaskazini Pemba. Zaidi ya tani 10,000 za mwani, huzalishwa kila mwaka.
Pamoja na kuwepo kwa kampuni 14 zinazonunua Mwani Zanzibar, bado bei yake hairidhishi na haiwezi kumkwamua mkulima kama ilivyokuwa ikitarajiwa. Miongoni mwa kampuni zilizopo ni CWEED Corporation Pemba, ambayo inatoa huduma za kununua MWANI pamoja na kutoa vifaa kwa Wakulima 200 wa MWANI, wanachama wao tu kisiwani Pemba.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya CWEED kisiwani Pemba, Hamil Said Soud ametaja mwa sababu zinazochangia bei ya mwani kuwa ndogo kuwa, ni kuporomoka kwa bei ya mwani katika soko la Dunia, pamoja na kuwepo kwa utitiri wa kodi.