Mkullo kama waziri wetu wa Fedha ni fedheha tupu kwani hajui hata mambo ya msingi ya kuendesha wizara hiyo kwa mfano ; chombo kama Benki kuu kiko chini yake na katika utendaji wake ili kiwe na tija kina regulations zake ambazo tunatarajia waziri wa fedha atazifahamu na kuziheshimu lakini si hivyo kwa Mkullo!! Kipengele 3,1[v] cha MWONGOZO WA BENKI KUU kuhusu wajumbe wa bodi kwenye mabenki unazuia wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wajumbe wa Baraza la wakilishi Zanzibar na madiwani kuwa wajumbe wa bodi katika mabenki yote nchini Tanzania. Mkullo kwa kuvunja kanuni hii amewateua Kaboyonga mbunge wwa Tabora mjini, DR. Kigoda kuwa wajumbe wa benki ya Twiga Bankcorp pia Nyami mbunge toka Rukwa ni mjumbe wa bodi ya NBC. Ukilaza wa namna hii wa Mkullo inaonesha dhahili kuwa hata hilo tawi la DECI inawezekana alilifungua huko kilosa ingawa sasa anabisha!!