Mkumbuke Meja Alexander Gwebe Nyirenda

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Posts
34,181
Reaction score
41,563

Kupanda kilele cha Mlima Kilimanjaro
Nyirenda ni mtu pekee ambaye kamwe hawezi kuachwa katika historia ya aina yoyote juu ya uhuru wa Tanganyika.
Ni yeye aliyepandisha mwenge wa uhuru na bendera katika mlima mrefu kuliko yote Afrika, wa Kilimanjaro Desemba 9, 1961.
Nyirenda alifanya kazi hiyo kwa ujasiri mkubwa, ikikumbukwa kuwa wakati huo, kupanda mlima huo ilikuwa ni jambo kubwa, zito na la hatari kutokana na ukweli kwamba kulikuwa na barafu nyingi na watu wengi waliogopa wakiamini kuwa uwezekano wa kurudi chini ukiwa hai ulikuwa mdogo.
Akielezea tukio hilo, Nyirenda alisema msafara wa kupanda Mlima Kilimanjaro ulikuwa na watu 11, wakiwemo wapiga picha na watangazaji wa redio.
Safari yao ilianza jijini Dar es Salaam kwenda Kilimanjaro ambapo walitumia jumla ya siku 16 kutimiza wajibu huo mzito.
Anasema kabla ya kuanza kupanda, walifanya mazoezi ya kupanda mlima na maandalizi mengine, kwa siku nyingi na siku hiyo walianza kupanda saa 12 jioni na kufanikiwa kufikia juu ya kilele majira ya saa tano usiku.
"Tulianza matayarisho ya kuweka mwenge huku tukiwasiliana na wenzetu wa Dar es Salaam kwa njia ya redio.
"Ilipofika saa sita kamili usiku wa Desemba 9, tuliwasha mwenge tukio ambalo lilikwenda sambamba na kupandishwa kwa bendera ya uhuru wa Tanganyika katika Uwanja wa Taifa wa Uhuru jijini Dar es Salaam," alisema Nyirenda

Kurejea Dar es Salaam
Baada ya kukamilisha shughuli ya kupanda Mlima Kilimanjaro na kuweka alama hizo muhimu za uhuru, walirudi Dar es Salaam, ambako mji ulikuwa bado ‘ukichemka' kwa shangwe na nderemo za uhuru kila kona.
"Tulipokelewa kwa furaha kubwa na Rais Nyerere ambaye alikuwa pamoja na mume wa Malikia wa Uingereza (Duke of Edinburgh) ambaye alikuwa amekuja nchini mahsusi kwa ajili ya sherehe za uhuru," alisema Nyirenda katika mahojiano yaliyofanyika miezi michache kabla ya kifo chake.
Nyirenda alieleza kuwa, Mwalimu Nyerere alikuwa mtu ambaye alijitolea kuwa mtumishi wa dhati, na aliyefanya yote sio kwa ajili yake binafsi bali wananchi wake.
"Alitufundisha kuthamini wengine kwa kuweka neno "sisi" na sio "mimi", yaani alitufundisha umoja, tuwe pamoja bila kutengana," alieleza Nyirenda.
Kuugua na kifo chake
Kama kuna jambo lililowasikitisha wengi, ni kutelekezwa kwa muda kwa shujaa huyu baada ya kuanza kuugua ugonjwa wa saratani.
Askari huyu shujaa, alianza kupata msaada wa serikali pale tu vyombo vya habari vilipoanza kuandika na kutangaza habari za kuugua kwake. Ni serikali hiyo hiyo iliyogharamia mazishi yake baada ya kufariki dunia.

Alifikia cheo cha Brigeia Jenerali kabla ya kustaafu rasmi jeshi.

My Take:

Je Historia ya nchi hii inamkumbuka? Wapo wengi waliojitolea kwa hali na mali kuipigania nchi yetu lakini historia imewakeka kando. Kizazi cha dot com kinajua chochte kuhusu shujaa huyu? nini kifanyike?

Habari kwa hisani ya Tanzania Daima.
 
Inasikitisha, kizazi cha dot com kazi yake kupika majungu tu mara diamond kafanya hivi mara lile
 
Inasikitisha, kizazi cha dot com kazi yake kupika majungu tu mara diamond kafanya hivi mara lile

... na wako bize katika kujifunza na kufuatilia historia za Manchester United, Liverpool, Chelsea, Real Maldrid, Barcelona, n.k.
 
... na wako bize katika kujifunza na kufuatilia historia za Manchester United, Liverpool, Chelsea, Real Maldrid, Barcelona, n.k.
facebook, twitter na blogs mbalimbali kama vile Diamond katoa kibao gani, anavaa nini, anaendesha gari gani nk Hawana muda wa kusoma historia kujua ni kina nani wamechangia nini kulifikisha taifa hapa lilipo.

Kizazi kinapukutika hiki na ni dalili za taifa lisilo na mwelekeo.
 
Kongolo ikiwa alistaafu kwa cheo cha brigedia jenerali iweje awe anaitwa kwa cheo cha meja?
 
Last edited by a moderator:
Kuna mtu alishawahi kuniambia kwamba historia ya huyu jamaa ilibidi iwekwe pembeni kwani baada ya kazi nzuri aliyofanya kumbe hakuwa mtanzania. Walikuja kugundua baadae kuwa ni mmalawi pamoja na kuwa alishaingia katika jeshi letu
 
TANZANIA Bwana kuna mengi mimi kilichonisikitisha sana ni hawa Wastaafu wa MAJESHI yetu wanavyoteseka na maisha wakati walitoa mchango mkubwa sana katika nchi hii,Nasikitika pia kusikia kuna mtu alimwambia kuwa Nyirenda ni mtu kutoka MALAWI??????Mbona watu hawamsemi OKELLO huko Zanzibar.tuache ubaguzi wa rangi hata kama yeye hakuwa raia wa nchi yetu kikubwa alitoa mchango gani kwa taifa letu??????
 
Hivi huyu anaundugu na kina nyirenda wa mbezi? Na yule dada uwt makao makuu?
 
Alifariki mwaka gani tafadhali.!!
 
Kuna mtu alishawahi kuniambia kwamba historia ya huyu jamaa ilibidi iwekwe pembeni kwani baada ya kazi nzuri aliyofanya kumbe hakuwa mtanzania. Walikuja kugundua baadae kuwa ni mmalawi pamoja na kuwa alishaingia katika jeshi letu
Mbona inasemekana wote waliokuwepo nchini wakati wa uhuru, moja kwa moja walihesabika ni watanzania? Kwa nini huyu alitelekezwa?
 
Mbona inasemekana wote waliokuwepo nchini wakati wa uhuru, moja kwa moja walihesabika ni watanzania? Kwa nini huyu alitelekezwa?

Duh,Kwa hiyo hata Governor wa mwisho wa kiingereza pamoja na Mume wa Malkia nae alihesabika Mtanzania (Mtanganyika) maana wote walikuepo siku ya uhuru?
 
Duh,Kwa hiyo hata Governor wa mwisho wa kiingereza pamoja na Mume wa Malkia nae alihesabika Mtanzania (Mtanganyika) maana wote walikuepo siku ya uhuru?
Ha ha ha
Mkuu umenifanya nicheke sana aiseee
 
Duh,Kwa hiyo hata Governor wa mwisho wa kiingereza pamoja na Mume wa Malkia nae alihesabika Mtanzania (Mtanganyika) maana wote walikuepo siku ya uhuru?

Ha ha ha haaah!! Nadhani kama wangetaka kuwa raia wa Tanganyika wasingezuiwa.
 
na ndio sababu wanakosa cha kuandika ktk mitihani yao na badala yake wanaamua kuchora mazombie, hopeless kabisa kizazi hiki.
 
ole! enyi kizaz cha nyoka,, angalieni sn, maana nyakat za mwisho zimekaribia.
 
Kongolo ikiwa alistaafu kwa cheo cha brigedia jenerali iweje awe anaitwa kwa cheo cha meja?

..Nyirenda alistaafu wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere akiwa na cheo cha Major.

..baadaye Raisi Mwinyi, kwa kutambua na kuenzi mchango wa Nyirenda, aliamua kumtunukia cheo cha Brigedia Jenerali.

NB.

..Jwtz ilipoanzishwa mkuu wa majeshi wa kwanza alikuwa na cheo cha Brigedia.

..Brigedia ni cheo kinacholingana na Brigedia Jenerali leo hii.
 
Yule Kijana wake pale Pepsi makao makuu ni MTU mwema sana.Thanks brother Alexander.
And sorry kwakumpoteza mama karibuni,sikujua mpaka nilipoona huu Uzi kwamba March 5 tulimpoteza.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mtu alishawahi kuniambia kwamba historia ya huyu jamaa ilibidi iwekwe pembeni kwani baada ya kazi nzuri aliyofanya kumbe hakuwa mtanzania. Walikuja kugundua baadae kuwa ni mmalawi pamoja na kuwa alishaingia katika jeshi letu
Ni kweli.Nyirenda ni jina la Malawi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…