Mkurugenzi Beatrice Kimoleta: TAMISEMI yafanya maboresho ya Sheria na Kanuni Mikopo ya Asilimia 10

Mkurugenzi Beatrice Kimoleta: TAMISEMI yafanya maboresho ya Sheria na Kanuni Mikopo ya Asilimia 10

OR TAMISEMI

Ministry
Joined
Jul 3, 2024
Posts
20
Reaction score
93
c2519c17-d857-43c5-851d-3a1fee99313f.jpeg

Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Beatrice Kimoleta amesema baada ya Serikali kutangaza kurejesha mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, Ofisi ya Rais – TAMISEMI imefanya masuala mbalimbali kuboresha mikopo hiyo kwa kufanya marekebisho ya Sheria ya Fedha sura 29, mapitio ya Kanuni za Mikopo ya asilimia 10, uandaaji wa Miongozo na Vitini vya mafunzo.

Pia amesema baada ya mafunzo hayo jumla ya wawezeshaji 840 watajengewa uwezo na baada ya hapo watakwenda kutoa mafunzo kwa Kamati za Uratibu wa mikopo ngazi ya Mikoa, Halmashauri na Kata kuhusu nafasi zao katika kusimamia utoaji wa mikopo ya vikundi.

Akitoa neno la shukrani Mkurugenzi wa Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Erick Kitali amemshukuru kwa mafunzo hayo na kuahidi kusimamia maelekezo yote ya Serikali yaliyotolewa kuhusu utoaji na usimamizi wa mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika ngazi zote.

Mafunzo hayo ya siku tatu yaliyozinduliwa leo Julai 9, 2024, ambapo yamehudhuriwa na baadhi ya Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Wawezeshaji wa Mafunzo, Wataalamu kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Pia, soma;

SoC04 - Mambo ya kuboresha katika utoaji wa mikopo ya asilimia 10% inayotolewa na halmashauri ili kufikia mapinduzi ya kiuchumi kwaka 10 ijayo nchini
 
Back
Top Bottom