Hai
Kwanza mimi siyo mwalimu, japo hutaamini; lakini hata kama ningekuwa mwalimu.
Haijalishi nimejiunga lini JF, haijalishi nimechangia mara ngapi; muhimu ni kwamba ninachoandika ni cha kweli, na ninachangia mijadala kama wewe ulivyochangia ili wahusika wachukue hatua kama mwanajamii.
Mwl. Mary Maganga alihamishwa kutoka Nyanguge kwenda Nyambitilwa kwa mgogoro na jamii.
Alihamishwa tena kutoka Nyambitilwa kuja Magu kwa mgogoro na jamii.
Kwa uongozi wake usiofaa, amesababisha watoto wawili kugongwa wakienda kuteka maji kwenye lambo.
Ana mgogoro na Kamati ya shule, mpaka wanakamati wamemsusia, kiasi kwamba hata ujenzi wa jengo jipya amesimamia peke yake. Kamati za shule zipo kimuundo wa wizara, siyo uamuzi wa DED, DEO, AEK, WEO wala mwalimu mkuu.
Anaongoza waalimu waliomzidi kitaaluma, hiyo inamfanya asijiamini na amekuwa kupeleka mashtaka mara kwa mara ofisi ya DEO na DED.
Ndivyo alivyo mwl. Mary Maganga unayesema ninamchora kila mara kwenye post zangu.
Huwezi kumsafisha kwa kuni-shoot mimi; hiyo ni historia aliyojitengenezea mwenyewe, haiwezi kubadilika.