Mkurugenzi JKCI: Kati ya watu takribani elfu 16,000 waliohudumiwa kwenye 'tiba mkoba', asilimia 25 wana magonjwa ya moyo

Mkurugenzi JKCI: Kati ya watu takribani elfu 16,000 waliohudumiwa kwenye 'tiba mkoba', asilimia 25 wana magonjwa ya moyo

informer 06

Member
Joined
May 11, 2024
Posts
66
Reaction score
49
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dr. Richard Kisenge amesema kuwa kupitia huduma ya tiba mkoba inayotambulika kama (Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Service), tayari imifika karibia mikoa 16 nchini na kuhudumia watu takribani elfu 16,000 ambapo kati ya watu hao asilimia 25 wamebainika kuwa na magonjwa ya moyo, huku kiwango kikubwa kikiwa ni shinikizo la damu (presha).

"Mpaka sasa hivi wananchi waliojitokeza kwenye mikoa tuliyopita wanafikia elfu 16,000 na asilimia 25 ndio walionekana kuwa na matatizo ya magonjwa ya moyo. Na tatizo ambalo lilionekana kuwa kubwa shinikizo la damu, ambapo wananchi wengi wameshapata maathiriko ya misuli ya moyo, misuli yao imetanuka kutokana na shinikizo la damu" amesema Dr. Kisenge

Amesema kwamba katika mikoa ambayo wamefikia, Mkoa wa Arusha ulikuwa na mwitikio mkubwa zaidi, pia mikoa mingine ambayo amedai imekuwa na mwitikio ni pamoja na Mkoa wa Dar es Salaam na Kilimanjaro, ambapo amedai kuwa katika waliofanyiwa vinufaika na huduma mkoani Arusha asilimia 40 walibainika kuwa na matatizo ya magonjwa ya moyo

Dr. Kisenge ambaye pia ni Daktari Bingwa wa maswala ya moyo ameyasema hayo Julai 6, 2023, wakati akibainisha wazi ushirikiano baina ya JKCI na ofisi ya Mbunge Jimbo la Namtumbo, Vita Rashid Kawawa, ambapo wanatarajia kushirikiana kuendesha huduma ya bure ya tiba mkoba kwa watoto na Watu wazima kuanzia Julai 8-13, 2024 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa 10 jioni katika kituo cha afya, Lusewa, Mputa pamoja na kwenye Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.
IMG_4496.jpeg

Pichani; Mkurugenzi wa JKCI, Dr. Richard Kisenge (katikati) akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Namtumbo, Vita Rashid Kawawa (kushoto) pamoja na Dr.Aaron Emilian (kulia)

Aidha akizungumzia mashirikiano hayo Mbunge wa Jimbo la Namtumbo, Vita Rashid Kawawa amesema kuwa katika Wilaya ya Namtumbo bado hawajawa na wataalamu wa kutosha ambao wamebobea katika kubaini matatizo ya moyo jambo ambalo wakati mwingine upelekea baadhi ya wananchi kutafuta njia mbadala hasa baada ya changamoto kushindwa kugundulika.

"Kama tunavyojua Wilaya yetu ya Namtumbo ipo mipakani na Msumbiji na tumekuwa na maradhi, lakini katika moja ya maradhi tunayoyapata mengine hatuyatambui, ni haya ya mishipa lakini pia na moyo, tuna madaktari katika vituo vya afya lakini wengi hawana taaluma hiyo kutambua mapema."amesema Mbunge huyo

Ameongeza"Kwahiyo wakienda wakatambua hayo magonjwa ya kawaida wanayatibu lakini wasipoyatambua haya wanamrudisha mgonjwa nyumbani, kwahiyo mgonjwa akirudi nyumbani, tuna utamaduni wa kiafrika kwenda kutafuta tiba mbadala kumbe shida ni magonjwa ya moyo"

Amesema kuwa katika kutafuta njia mbadala wakati mwingine imekuwa ikipelekea athari kubwa zaidi ikiwemo vifo. Ambapo amedai kwamba ujio wa JKCI utatoa fursa kwa wananchi kujua afya zao hususani yanayogusa matatizo ya moyo kwa ujumla bila kugharamia chochote.
IMG_4497.jpeg

Kwa upande wa Dr.Aaron Emilian Hyera, ambaye ni Mkuu wa divisheni ya Afya Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe, amesema kuwa kwa upande wa Namtumbo wanaoonekana kuwa na changamoto zaidi ya magonjwa ya moyo ni watu wazima kuanzia miaka 40 na zaidi, hata hivyo naye amedai bado kuna uhaba wa wataalamu katika nyanja hiyo.

Ambapo ameongeza kuwa baadhi wamekuwa wakipatiwa matibabu lakini inapobidi wanawapatia rufaa, japo kuwa amedai kuwa baadhi yao wamekuwa na changamoto ya kumudu gharama za matibabu pamoja na usafiri pale wanapopewa rufaa.

Amesema kwa wale ambao walikosa kumudu gharama mara baada ya kupewa rufaa ujio wa JKCI kupitia huduma mkoba watapa fursa ya kukutana na wataalamu ili kuweza kupatiwa huduma za kiuchunguzi.

Pia ameeleza tija ya elimu ya lishe ambayo itaambatana na huduma ya magonjwa ya moyo kama ambavyo imekuwa ikifanyika maeneo mengine, amedai kuwa inaenda kuongeza wigo zaidi kwenye hatua ambazo tayari wameendelea kuzipiga ili kuwaweka wananchi katika mazingira rafiki ya kuepukana na baadhi ya magonjwa yasiyoambukiza.

"Kwa utapiamlo katika Wilaya yetu tuna zaidi ya asilimia 33 ambazo pengene ni zaidi ya kiwango kile cha Kitaifa, hivyo elimu hii ya lishe sasa ni muhimu sana" amesema Dr.Aaron

Katika hatua nyingine ili kukabiliana na magonjwa hayo, Dr. Kisenge amesisitiza umuhimu wa wananchi kufanya mazoezi na kuepuka matumizi ya sukari kwa wingi pamoja na ulaji bora wa vyakula ambavyo vinawaweka katika mazingira ya kuepuka magonjwa ya moyo.
 
Back
Top Bottom