Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Wakati Novemba 27, 2024 ikiwa ni zoezi la kupiga kura kwa ajili ya kuchagua viongozi wa serikali za mitaa, mkoani Kigoma tangu asubuhi kumeshuhudiwa malalamiko ya uwepo wa kura feki licha ya wimbi la wananchi kuonekana kujitokeza kupiga kura.
Hali hii imeshuhudiwa katika maeneo ya Mwandiga, ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma ambako mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amekamatwa na kura feki 800. Katika Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani humo, kituo cha Masanga Stendi, baadhi ya wanawake wamekamatwa na kura feki wakiwa wanaingia nazo kituoni. Halikadhalika malalamiko yameshuhudiwa katika vituo vya Kamara, Bangwe, Kibirizi na maeneo mengine.
Kutokana na hayo, Jambo Tv tumemtafuta Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ambaye pia ni Msimamizi wa Uchaguzi katika eneo hilo Kisena Mabuba ambapo amethibitisha kuwepo kwa kura hizo feki.
"Zoezi linakwenda vizuri. Kuna uwepo wa kura feki ambazo hazifanani na za kwetu, na tayari tumeshachukua hatua, tayari kuna mtu mmoja tunamshikilia", ameeleza.
PIA SOMA
- LGE2024 - Kigoma: Kura feki zakamatwa Mwandiga