Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) ana mtihani mkubwa sana akifanikisha hili anastahili tuzo

Huyo jamaa unaesema ilitakiwa apewe tuzo,kwa nchi zinazofuata vizuri utaratibu wa sheria ilitakiwa awe jera kwa kuharibu mfumo mzima wa kibiashara nchini. Mfumo huu wa kuwabambikia kodi kubwa,kuwafungia na kuwavuruga kwa ujumla wafanyabiashara ungeendelea ndani ya miaka mi5 tena mbele,serikali ingekosa kabisa sehemu ya kukusanya mapato
 

Sasa ujanja mpka tufunge biashara zetu au mpaka tufilisike.Usikoment kitu usichokijua unakuwa kama unaugua fistula ya kichwa.
 
Mkuuu unaijua kkoo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Mbon majengo mapya hayajakamilika vizur n vyumba vimesha kodishwa vyote???
 
Mkuu suala la zile mashine za EFD kuuza gharama ni sahihi zilikuwa bei Sana , ziliuzwa hadi 2.8m. halikuwa kisingizio kabisa Mkuu,
 
Apunguze kodi Ili akusanye zaidi.
Gari japan dola 5000 kodi Bandarini dola 6000 utapata vipi kodi nyingi sasa.
 
Kwa nchi hii kiuhalisia inafundisha yenyewe ujanja watu. Mifumo haikupi uhuru wa kulipa kodi kiuhalisia. Mfano tuanze na hiyo mashine. Wakati zinaingia wakadanganya kwamba nunueni hizo mashine then mtarudishiwa kidogo kidogo kwenye kodi,lakini sina uhakika kama wapo hata mmoja alierudishiwa.
Halafu mashine zenyewe ni gharama. Laki 8. Haijalishi una mtaji wa kiasi gani. Kiuhalisia hizi mashine,ksbb wewe serikali unataka watu waingie kwenye huo mfumo,basi wagawie bure watu. Ili uwavute waingie kwa wingi,wagawie bure,andaa mazingira ya utengenezaji hizo kila mahala ziliko.
Sasa hizo mashine ukishanunua laki 8.,bado matengenezo ni juu yako. Kwa mfano wilayani kote hakuna mafundi wa hizo mashine. Ikiharibika lazima ufunge duka ukaitengeneze mkoani. Unafika kule mkoani inabidi uisubiri mpaka itengemae unakuta siku 2. Fikiria hizo gharama. Na mashine zenyewe mbovu zinaharibika haribika. Ukija upande wa risit,ukitoa risit 100% lazima ufirisike kwa mfumo wetu. “Nimechoka kuandika mkuu,nitarudi nikuambie kwa nini ufirisike”
 
wewe huelewi chochote subiri mshahara wako mwisho wa mwezi ambao unaupata bila kutoa jasho huku wanafunzi unawafundisha wanamaliza la saba bila kujua kusoma na kuandika
 
wewe huelewi chochote subiri mshahara wako mwisho wa mwezi ambao unaupata bila kutoa jasho huku wanafunzi unawafundisha wanamaliza la saba bila kujua kusoma na kuandika
Sawa mkuu
 
Apunguze kodi Ili akusanye zaidi.
Gari japan dola 5000 kodi Bandarini dola 6000 utapata vipi kodi nyingi sasa.
Dawa ni kuongeza vyanzo vipya vya kodi.
Ila habari ya kucheka na wafanyabiashara itaturudisha kule kwenye mishahara tarehe 40.
 
Nakubaliana na wewe kwenye kutoa bure mashine za EFD tena zifike hadi kwa wauzaji magenge na ikiwezekana hata frequent maintenance iwe ni jukumu la TRA.
 
Nadhani kitu kinachokosekana kwa wafanya biadhara wengi ni elimu ya kodi nina mwaka wa nne nikifanya biashara ya kusupply vitu mbali mbali kwa kuomba tenda kwenye makampuni na taasisi za serikali na binafsi ,kinachonisaidia ni elimu kubwa ya kodi niliyonayo na TRA wananifahamu myukano unakuwa mkubwa sana ujinga wowote unapoletwa kwenye kazi yangu ,sijawai kuongezewa wala kupunguziwa kodi,wala kuumizwa na kodi ,tunakwenda sawasawa .Nachotaka kujua kwanini ukitoa risiti unafirisika? Wakati kiuhalisia sio wewe unaelipa kodi Bali wateja wako?
 
Dawa ni kuongeza vyanzo vipya vya kodi.
Ila habari ya kucheka na wafanyabiashara itaturudisha kule kwenye mishahara tarehe 40.
Kodi iwe reasonable inayolipika na isiwe komozi.Chukua kidogo Ili kesho uchukue tena kuliko kukausha damu yote unapata nyingi mara moja ila kesho upati tena.Pili kodi ikiwa kubwa usababisha ukwepaji Kodi kuwa Mkubwa.
 
Lazima tuangalie wapi tulipo kosea. kuna mambo matatu. la kwanza . zamani bandalini ujanja unjanja ulikuwa Mwingi sasa wamethibiti ilikuwa wanakuletea kontena mpaka nyumbani kutoka bandalini bila lisiti.pia ukwepaji wa kodi ulikuwa mkubwa sana . ukizoea vya kunyonga vya kuchinja huviwezi. jambo la pili kodi kubwa za bandali ni tatizo kubwa wapunguze. tatu ruswa ndio adui mkubwa Bandarin na TRA. serikali impunguzie Mfanyabiashara kodi kuanzi bandarini hadi Tra.
 
Wawe wakweli juu ya biashara zao,pia walipe kodi kwa hiyali pasipo kusubiri task force!
 
Ni kweli bongo voluntary compliance level iko chini sana kuliko maelezo, sasa wanapotaka kuzuia level of enforcements iwe chini kabisa maana yake itaweza kupelekea hali ikawa worse ktk makusanyo.

Advanced countries level of voluntary compliance iko juu sana kiasi kwamba haihitaji enforcements efforts kubwa katika kukusanya mapato ya serikali.

Mleta mada una hoja ya msingi isipokuwa hujagusa hasa mambo ya msingi.

Hata hivyo umethubutu.
 
CAG amesoma report,, naamini umeisikia. Madudu chini ya uzalendo yaliyokuwa yanafanyika ni funga mwaka.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Kama ameweza kujenga miradi ya trillions of money,kukarabati shule na vyuo kongwe,kujenga vituo vya afya,masomo,vituo vya mabasi,hospital za wilaya,hospitali za mikoa na kanda,ukarabati wa meli,kununua ndege 11,kujenga miundo mbinu nyingi,na kulikuwa na upigaji ule basi niishie tu kusema jamaa alikuwa shujaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…