Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) ana mtihani mkubwa sana akifanikisha hili anastahili tuzo

Sasa ujanja mpka tufunge biashara zetu au mpaka tufilisike.Usikoment kitu usichokijua unakuwa kama unaugua fistula ya kichwa.
Ujanja ni nyie kufanya janja janja na kukwepa kodi?.Usikoment kitu kwa kuangalia upande wako unakuwa kama unaugua tezi dume ya kichwa!
 
Eti mfanyabiashara badala ya kuwasilisha VAT serikalini kwa wakati badala yake wanafanya udanganyifu kwa kutumia ghost receipts za manunuzi za kugushi ili wasilipe VAT [emoji848][emoji848]

Wakaenda mbali zaidi kwa kudai refund toka serikalini , fikiria [emoji848][emoji848]

Yani kuna wafanyabiashara walikuwa wanaiibia serikalini mara mbili.

Kwanza VAT alokuwa awasilishe serikalini hapeleki na anajifanya kudai refund kwa hiyo wizi mara 2.

Sasa kwa muktadha huo maelekezo yakitolewa kurudi miaka 8-10 nyuma kuna tatizo gani hao watu kukaguliwa na kurudisha pesa za Umma alizoiba kwa maslahi ya Umma?

Tusidanganyike wafanyabiashara nawashauri tuzingatie compliance jamani.
 
Tena wafanyabiashara wakijisahau wakaacha kulipa kodi stahiki wajue wakati utakuja hali ya hewa itakapobadilika na upepo wa kimbunga ambapo anaweza kuja kiongozi kama yule akaelekeza kurudi miaka 10 nyuma au zaidi .

Na mimi nitamuelewa kwa kuzingatia na kutanguliza maslahi ya Umma mbele.

Tutafakali sana.
 
Wewe ni tumbili tu.
Unajua kuandika hilo neno EFD kwa sababu wazazi wako walijifunga mkanda wakakupeleka shule.
We Baba yako huko kijijini amesoma wapi?Mama yako amesoma wapi?

Elimu ya Wafanyabishara siyo hiyo ya kwako ya square root...

Halafu ukute Baba yako pengine ni Kinyozi na anatumia umeme ambao unakatika kila baada ya masaa mawili,nikuulize,kazi ya kusambaza huo Umeme ilikuwa kazi ya Baba yako?

Hayo maumivu ya kukosekana kwa Umeme ambayo ndo biashara msingi ya Baba yako nani anamsaidia?
Ni kosa la nani?
Kwani huo si mfano mdogo tu...?

Ati mjanja mjanja!!!

People like you are like monkeys on the trees.....!
 
Kuna jamaa mmoja Mpemba kariakoo anauza vifaa vya umeme kwa bei ya jumla. Hata ukinunua vifaa vya milioni 3 lazima akupe risiti ya EFD wafanyabiashara wote wangekuwa kama huyu TRA wasingesumbuka kufungia biashara za watu

 
Kufanya arguments na wewe ni upumbavu wa hali ya juu,ulichokiandika inaonesha kabisa wewe ni mtu wa mipasho asie na lolote kichwani,na shule ambayo wazazi wako walikupeleka ni ya kujifunza mipasho na nyimbo za taarabu so huwezi jenga hoja zaidi ya kutukana ukizani kwamba ndo suluhisho la upungufu wako wa akili kichwani!
 
Kulipa Kodi ni lazima sio ombi..!
Tukianza kuchukulia kama kulipa kodi sio lazima tutayumba kama Taifa.

Naomba kukuomba uweke mapungufu waliyonayo Wafanyabiashara kwenye kulipa kodi.
 
Wanaokwepa kodi asilimja kubwa wanajua kuwa wanatakiwa kulipa kodi
 
Kodi iwe reasonable inayolipika na isiwe komozi.Chukua kidogo Ili kesho uchukue tena kuliko kukausha damu yote unapata nyingi mara moja ila kesho upati tena.Pili kodi ikiwa kubwa usababisha ukwepaji Kodi kuwa Mkubwa.
Kwani kuna kodi ambayo haikuwepo kipindi cha JK imekuja kuibuka kipindi cha Magu?
 
Kwani kuna kodi ambayo haikuwepo kipindi cha JK imekuja kuibuka kipindi cha Magu?
Nakumbuka Magufuli alikaa na wafanyabiashara wote, pia alikaa na watu wa madini. Walitoa mapendekezo yao na yalifanyiwa kazi. Hawa wengi wanaolalamika in wakwepa kodi janja janja nyingi.
 
Kuna siku nilikuwa kwa muhindi mmoja k/koo. Dukani pale nilinunua feni, pasi ya umeme na vitu vingine vichache jumla ilikuwa kama laki 2.2
Baada ya kuniwekea kwenye mfuko naona muhindi anajizungusha tu, Mimi nimetulia namuangalia mwisho wake, naona akashtuka akanipa risiti ya EFD yenye thamani ya elfu 20 na tarehe ya nyuma. Nikamwambia hii sio yangu naomba risiti yangu. Akaanza Boss hivi vitu tumekupunguzia bei sana blah blah kibao ila nikakomaa nae
 
Deni la Taifa limeongezeka tshs ngapi?
 
Kwani kuna kodi ambayo haikuwepo kipindi cha JK imekuja kuibuka kipindi cha Magu?
Nyingi tu zimebuniwa kwenye vyanzo vile vile vya kodi.Hadi wafanyabiashara wakakimbia nchi,labda kama wwe ni mgeni.
 
Huu ndiyo ukweli, asilimia kubwa ya wafanyabiashara hawalipi kodi.
 
uzuri anaeumia ni mwananchi mfanyabiashara anaangalia faida yake 18% unalipia mnunuzi
 
Pitia ripoti ya CAG utaona hata mashirika na taasisi za serikali "zinakwepa" kodi! Sisemi ni jambo zuri ila kodi inatakiwa ilipike....zikiwa kubwa mno kiliko uwezo wa watu kilipa ni tatizo (hii hata JPM alilisema na karibu Rais wa ZnZ.....)

Ni kweli CG ana kazi kubwa.....sheria zipo azitumie kwa busara ili na kesho kuwe na sehemu ya kukusanya. Hakuna maana kukusanya kodi nyingi leo na hapo hapo unauwa biashara na kupoteza ajira za watu......
 
Nyingi tu zimebuniwa kwenye vyanzo vile vile vya kodi.Hadi wafanyabiashara wakakimbia nchi,labda kama wwe ni mgeni.
Nitajie kodi ambayo haikuwepo kipindi cha JK ikaja kuletwa kipindi cha Magu
 
Nakuelewa vizuri lakini kumbuka bila nchi kukusanya kodi inayotoshereza haiwezi kwenda!
 
Reactions: SMU
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…