LGE2024 Mkurugenzi na Msimamizi Uchaguzi Michael Gwimile: Prof. Jay amepotosha, Uchaguzi Serikali za Mitaa utakuwa wa haki

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu, safari hii mambo ni moto kwelikweli! Ripota wenu, Cute Wife, kama kawaida nawasogezea taarifa ili siku ya kupiga kura mfanye maamuzi sahihi.

Mkurugenzi na Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Kilosa, Michael John Gwimile, amesema kuwa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Kilosa, Joseph Haule (Prof. Jay), ni ya uongo na inalenga kupotosha umma.

Bongo 5.jpg

Profesa Jay alizungumza kwenye kipindi cha Power Bank akilaani kitendo cha majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuenguliwa. Akijibu kuhusu madai hayo, Gwimile amesema:

"Kwa data tulizonazo mpaka siku ya mwisho tulipopokea fomu za wagombea, kwa nafasi ya wenyeviti wa vijiji CHADEMA waliomba jumla ya nafasi sabini. Tafsiri ni kwamba, kati ya vijiji tulivyo navyo 138 ndani ya Wilaya ya Kilosa, chama hicho kiliomba nafasi sabini pekee, ambazo ni takriban asilimia 50 ya vijiji vyote.

Soma pia: Joseph Haule 'Prof. Jay: Nitagombea Ubunge Mikumi 2025

“Ukija kwa upande wa vitongoji, tuna jumla ya vitongoji 818 ndani ya wilaya hii. Hawa CHADEMA wameomba nafasi 282, na kwa uchaguzi huu vyama vilivyo omba nafasi kwa ujumla vipo 12. Kwa hiyo, nikiwa kama Mkurugenzi hapa, naomba nitoe taarifa rasmi kwamba hicho kilichopostiwa na Prof. Jay kuhusiana na wagombea wao kuenguliwa si sahihi; kwa hiyo, hakuna jambo kama hilo.

“Huu uchaguzi ni wa kila mtu, na vyama vilivyojitokeza vitapata haki mpaka siku ya mwisho. Lengo letu ni kwamba huu uchaguzi uende kuwapatia wananchi viongozi wanaowataka kwa ajili ya kuwaletea maendeleo kwa miaka mitano kuanzia sasa," amesema Gwimile.
 
Attachments

  • Screenshot_20241109_103511_Firefox.jpg
    Screenshot_20241109_103511_Firefox.jpg
    261.9 KB · Views: 4
Data zinaongea.

Chadema kubalini hamjajipanga kwa ngazi za chini kuliko watu.

Mmejazana mitandaoni tu na kwa wahuni WA mijini.
 
Mkurugenzi, acha shwaga zako wewe! Tunajua jiwe ndio aliwajaza ujinga Kwa kukiuka katiba! Mpumbavu yule! Yuko kuzimu Sasa!
 
Data zinaongea.

Chadema kubalini hamjajipanga kwa ngazi za chini kuliko watu.

Mmejazana mitandaoni tu na kwa wahuni WA mijini.
Duh aisee nawaza kwa roho mbaya kama hii na chuki uliyonayo dhidi ya wasiokuwa CCm je itakuwaje siku ukija kuwa kìongozi?kwasababu mwenye akili timamu ilibidi asishabikie upande bali atumie akili zake kuangalia ukweli wa hilo
 
Back
Top Bottom