Mkurugenzi wa Barrick, Mark Bristow atua nchini, aonana na kumpongeza Rais Samia. Je, kutua 77 Banda la Barrick?

Mkurugenzi wa Barrick, Mark Bristow atua nchini, aonana na kumpongeza Rais Samia. Je, kutua 77 Banda la Barrick?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Serikali na Barrick zathibitisha umuhimu wa kushirikiana

Dodoma, Julai 7, 2021 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amekutana na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick Gold Corporation (NYSE:GOLD)(TSX:ABX), Mark Bristow

jijini Dodoma ili kutathmini mafanikio ya kampuni ya madini ya Twiga (Twiga Minerals Corporation) pamoja na mustakabali wake. Kampuni hiyo ya Twiga ni zao la ubia kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania.

Kampuni ya Barrick iliingia katika ubia na Serikali ya Tanzania mwezi September, mwaka 2019. Tangu hapo ilijikita katika kufufua na kukuza uzalishaji katika migodi ya North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi. Kwa hakika, jitihada hizo za ubia zilizaa matunda na hivi sasa migodi hiyo inazalisha faida na imefikia viwango vya kimataifa katika uzalishaji na uendeshwaji wake. Hali hii ikiendelea itaiwezesha migodi hiyo kuwa katika orodha ya migodi saba ya Barrick duniani kote kufikia hadhi ya daraja la juu kabisa la uzalishaji wa dhahabu (Tier One1 Gold Complex). Pamoja na jitihada kubwa ilizoziweka katika uzalishaji wa dhahabu, kampuni ya Barrick pia imepiga hatua kubwa katika kuzitatua changamoto mbalimbali za kijamii na zile za mazingira ili kurejesha thamani ya biashara kwa watanzania.

Mwaka 2020 Serikali ya Tanzania ilipokea kiasi cha Dola Milioni 370 (sawa na Shilingi Bilioni 856 za Kitanzania) kama malipo mbalimbali yaliyotokana na mafanikio ya ubia huu wa Twiga. Malipo hayo yalijumuisha kodi na tozo mbalimbali, gawio la faida, pamoja na awamu ya kwanza ya malipo ya maafikiano (settlement agreement) ya Dola Milioni 100 ambayo ni sawa na takriban Shilingi Bilioni 231 za Kitanzania. Aidha, kampuni ya Barrick imewekeza Dola Milioni 800 (sawa na Shilingi Trilion 1.851 za Kitanzania) katika uchumi wa nchi na kutumia kiasi cha Dola Milioni 2 (sawa na Shilingi Bilioni 4.6 za Kitanzania) katika masuala mbalimbali ya kijamii.

Kwa upande wa raslimali watu, Bristow alimueleza Rais kwamba Barrick, imetengeneza ajira mpya 600. Hatua hii imefanya asilimia 96 ya wafanyakazi wote migodini kuwa ni Watanzania. Kampuni pia imewateuwa watanzania kushika nafasi za juu katika uongozi wa kampuni hiyo hapa nchini ambao ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara – Apolinary Lyambiko; Meneja Mkuu wa Nchi – Georgia Mutagahywa pamoja na Meneja Mkuu anayesimamia masuala ya Fedha na Utawala– Melkiory Ngido.

Katika jitihada zake za kuhakikisha wazawa wananufaika na biashara zitokanazo na uwepo wa migodi yake nchini, Barrick inafanya kazi kwa ukaribu mkubwa na Tume ya Madini ili kukuza idadi na uwezo wa makampuni ya ndani ya nchi kutoa huduma mbalimbali katika sehemu hizo. Hadi kufikia robo ya pili ya mwaka 2021, asilimia 73 ya malipo ya manunuzi ya vifaa na huduma mbalimbali katika migodi hiyo yamefanyika kwa makampuni ya ndani.

Aidha, Bristow alisema mkutano wake na Rais Samia Suluhu Hassan ulikuwa mzuri sana na kwa pamoja wote walikiri kwamba mafanikio ya ubia wa Twiga, ambao ni wa kwanza barani Afrika, ni wa kuigwa kwani umedhihirisha kwamba ushirika baina ya migodi na nchi, huleta manufaa makubwa ya kiuchumi kwa pande zote mbili.

“Nimemhakikishia Rais Samia Suluhu Hassan kwamba kampuni ya Barrick imedhamiria kuendelea kuwekeza nchini Tanzania. Katika hili, tutaitumia migodi yetu ya North Mara na Bulyanhulu kwa pamoja kama sehemu ya kuuendeleza uwekezaji huo kwani tunaona uwezekano mkubwa wa uwepo wa madini katika maeneo ambayo hadi hivi sasa bado hayajafanyiwa utafiti. Hivyo basi, tutaendelea kuomba leseni mpya za uchimbaji kwani, ilituweze kufanya utafiti wenye matokeo chanya, tunahitaji kuendelea kupata maeneo mapya kwa ajili ya utafiti na uchimbaji,” alisema Bristow.

Swali kwangu ni. Je Guy jamaa atatinga Saba Saba banda la Madini ambamo Barrick wamo?, Ikitokea akatinga, Jee tutapata fursa ya kumuuliza maswali?. Maana Nina swali moja, fulani kuhusu île 50/50 ya faisait.

Paskali
 
Itakuwa amekuja kufatilia Makinikia yake yaliyozuiwa pale Bandarini kutokana na maagizo ya Serikali iliyopita.

Ndani ya siku 100 ya utawala wake, Mhe. SSH ameweza kurudisha mahusiano mengi ya ndani na nje ya Nchi yaliyodolola kwa kipindi chote cha awamu ya 5.

Mitano tena kwake👏👏👏👏
 
Nilisikiaga ni yeye na timu yake majitu yaliyobibea kwenye ujasusi duniani.Mama ajihadhari na wanasheria mahili kukabiliana nao kwenye mkataba wowote ule.
 
CCM Mpya ya wana Lumumba ilee, mtambue, Huwezi kushindana na wenye mitaji.
Hatua hii ya mwenyekiti wa 'CCM ya kweli / asilia ' ambaye ni Mh. Rais Samia Suluhu Hassan wamechagua kuchukua hatua sahihi katika kufanya kazi na wadau wa maendeleo , wawekezaji na Jumuiya ya kimataifa.


Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Akutana na Kuzungumza na Afisa Mtendaji Mkuu Makampuni ya Barrick Gold Bw. Mark Bristow


1-1-1024x531.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu Makampuni ya Barrick Gold Bw. Mark Bristow Ikulu Jijini Dodoma leo Julai 07,2021
 
Back
Top Bottom