Mkurugenzi wa Grace Products atwaa tuzo ya Super Woman kutoka Wasafi Media

Mkurugenzi wa Grace Products atwaa tuzo ya Super Woman kutoka Wasafi Media

Ambakucha

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2019
Posts
317
Reaction score
520
Mkurugenzi wa Kampuni ya Grace Products, Dk. Elizabeth Nyamizi Kilili, jana Jumanne, Machi 8, 2022 alitwaa tuzo ya Super Women katika hafla kubwa iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Dk. Elizabeth ametwaa tuzo hiyo iliyotolewa na waandaaji, Wasafi Media katika Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 8 ya kila mwaka.

Huu ni mfululizo wa kutwaa tuzo tangu 2017 alipotwaa Shahada ya Uzamivu ya Public Administration & Business Management kutoka Chuo Kikuu cha Africa Graduate University na ndipo alipoanza kuitwa Dk.

June 29, 2018 aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hayati Dr. John Pombe Magufuli alimpongeza Dk. Elizabeth Kilili kwa kutumia lugha ya Kiswahili wakati akipokea Tuzo ya Ubora wa Viwango vya Kimataifa nchini Marekani akizipiku nchi 116 alizoshindanishwa nazo.

Hayati Magufuli aliandika katika ukurasa wake wa Twitter; “Nimefurahishwa na ushindi wa Grace Products, lakini pia nimefurahishwa kwa kutumia Kiswahili kukizungumza nchini Marekani, hongereni sana Grace Products.”

Aidha, 2017, Dk. Elizabeth alitwaa Tuzo ya Malkia wa Nguvu, waandaaji wakiwa Clouds FM.

Kwa mujibu wake, heshima anayoipata sasa katika jamii ni baada ya mateso na mahangaiko mengi sambamba na kejeli katika kutafuta.

"Nimepitia magumu, siku si nyingi nitayaanika hadharani watu wajue maana haikuwa rahisi kufika hapa nilipo," alisema Dk. Elizabeth.

IMG-20220310-WA0011.jpg
 
Huyu mbona amepotea na 'zoazoa' yake
 
Back
Top Bottom