Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Maxence Melo amesisitiza suala la JamiiForums kutaka kujitanua na kuzifikia nchi nane za Afrika ili kuwapa watu wa nchi hizo huduma ambayo watanzania wamekuwa wakiipata pia kukuza Kiswahili.
Suala la umuhimu wa faragha ni suala alilozungumza kwa undani akitaja mfano wa watu kuandika majina wanapoingia katika nyumba za wageni nk hali inayofanya taarifa za watu kuzagaa hovyo bila kuwa na sheria ya kulinda faragha za watu.
Faragha ya mtu ndio utu wa mtu.
Faragha za watu
Maxence Melo amezungumzia suala la watu kupiga picha bila ridhaa na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii. Ametolea mfano suala la mtu kuwa kwenye sherehe au tafrija ambapo baadhi ya watu huwa na kawaida ya kuchukua video na kuzipost kwenye mitandao ya kijamii bila ruhusa ya aliowapiga picha