upupu255
Senior Member
- Sep 4, 2024
- 119
- 144
Habibu Mchange, Mkurugenzi Mtendaji wa magazeti Jamvi la Habari, Times Observer, Tanzania Bora na mengineyo amedaiwa kushikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kigamboni kwa saa kadhaa.
Inadaiwa kuwa Mchange aliitwa TAKUKURU Ijumaa saa tatu asubuhi baada ya siku ya Alhamisi kukaa ofisini hapo hadi saa saba usiku.
Tukio hili limejiri muda mfupi baada ya magazeti yake kuandika habari za taasisi hiyo kuwafungia ofisini viongozi wa CCM kata ya Tungi iliyopo wilaya ya Kigamboni.
Soma, Pia: Mambo yafichuka ndani ya Equity Bank, mmiliki wa gazeti la Jamvi la Habari alipewa tender na swahiba wake Zenda
Inaelezwa kuwa baada ya viongozi hao kufungiwa ofisini, Mchange na wanahabari wenzake walikimbilia eneo hilo na kusimamisha gari lao mita chache mbele ya ofisi na liliposimama gari la TAKUKURU, wakifuatilia kinachoendelea. Baada ya hapo maafisa hao waliwaamuru waongozane nao hadi ofisini kwao.
Jambo TV imepata kuwasiliana na afisa fulani ndani ya TAKUKURU Kigamboni ambaye ameeleza kutokuwa na mamlaka ya kulisemea jambo hilo, bali mwenye mamlaka hayo ni Mkuu wa TAKUKURU wilayani humo ambapo jitihada za kuwasiliana naye bado zinaendelea.
Chanzo: Jambo TV