Mtoa Taarifa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2024
- 213
- 671
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Jatu PLC, Peter Gasaya (33), anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashitaka mawili likiwamo la kujipatia Sh5.1 bilioni kwa njia ya udanganyifu, amefikisha siku 690 akiwa gerezani kutokana na upelelezi wa shauri hilo kutokamilika.
Mbali na upelelezi kutokamilika, mshtakiwa huyo kupitia wakili wake, Nafikile Mwamboma ameiomba Mahakama hiyo imfutie kesi mteja wake na imuachie huru.
Gasaya anadaiwa kujipatia fedha hizo kutoka katika Saccos ya Jatu kwa madai kuwa fedha hizo atazipanda kwenye kilimo cha mazao ili kuzalisha faida zaidi, wakati akijua kuwa ni uongo.
Kwa mara ya kwanza, Gasaya alifikishwa mahakamani hapo Desemba 29, 2022 na kusomewa mashitaka yanayomkabili.
Hata hivyo, tangu afikishwe mahakamani hapo hadi leo Jumatatu Novemba 18, 2024 amefikishwa siku 690, sawa na mwaka mmoja, miezi 10 na siku 20 akiwa gerezani kutokana na upelelezi wa shauri hilo kutokukamilika.
Wakati mshtakiwa akifikisha siku hizo bila upelelezi kukamilika, upande wa mashitaka umedai kuwa bado unaendelea na upelelezi wa shauri hilo.