DOKEZO Mkurugenzi wa Jiji Dodoma fuatilia watoza huduma maegesho wako!

DOKEZO Mkurugenzi wa Jiji Dodoma fuatilia watoza huduma maegesho wako!

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
12,675
Reaction score
25,924
Niliamua kutembelea waifu kwa wiki kama 2 Dodoma nimegundua kitu fulani cha ajabu sana kwenye maegesho ya magari Dodoma.

1. ukiegesha gari, mtu anakuja kuscan namba ya gari, hata dakika chache hazijafika mwingine anafanya hivyo. nilipouliza mmoja akaniambia wanaweza kuscan 500 hadi 3000. nikajiuliza, control mechanism ni ipi? manake nilitegemea labda mtu mmoja akiscan 500 inakuwa ni kwa siku nzima, kumbe la, yeyote anayepita akijiskia anakuscan na kukupa deni. na hakwambii amekuwekea bei gani.

2. Wanaomba sana pesa. wanakuja dirishani kwako wanakwambia kama unataka wasiscan uwape walau jero. ukikataa (manake sisi wengine hatutoi rushwa ni dhambi), wanakwambia basi ngoja tuscan, na anaposcan anascan kwa bei ya juu as if unapaki siku au wiki nzima sijui, anafanya kwa hasira kwasababu umegoma kumnpa jero.

3. kwa nini msiweke utaratibu, zile mashine zenu akiscan zitoe risiti hapohapo, ili kujua kwa siku nimetozwa bei gani? manake kuna wengine kulingana na utakavyoelewana na mkaguzi unaweza ukalipa, wengine wanalipa watalipa 500 wengine 3000. just per day.

4. kuna siku mtasababisha ugomvi mkubwa sana na mtu asiyeelewa hili jambo kwa sabaub mnakera sana sana.

Mkurugenzi wa Jiji, fuatilia hili, ninakupa maelekezo, kama hautafuatilia hili yatakutokea puani.
 
yaani kila nikienda dodoma siishiwi kero. wakati mwingine watoza ushuru wao wa stand ya nanenane, wanakutozeni ushuru wa kuingia na gari, ticket unayo ila ukishushwa ukapande basi pale mlangoni uwe na ticket au hauna utatozwa tena. sasa huu ni wizi wa wazi kabisa, serikali imeishiwa hela namna hii hadi iwe inapora kwa wananchi?
 
Unamiliki gari la mamilioni unalalamikia gharama za maegesho? Aibu nyingine hizi zitupite tu
 
Unamiliki gari la mamilioni unalalamikia gharama za maegesho? Aibu nyingine hizi zitupite tu
ndio mzee, mimi huwa sipendi hela yangu iende bure, hasa kama inaenda kwenye serikali yenye rushwa. si bora nikatoe sadaka au niwapa maskini mtaani.
 
Punguzeni shobo
of course sio kwamba nashindwa kulipa maegesho Tzs 3000 kwa siku, niliudhika kwanza wanapoanza kuomba pesa badala ya kuscan, na pili najua kuna wengi tu humu hiyo inaweza kuwa mzigo, tunapoweka hoja hapa tunaweka sometimes kwa manufaa ya wengi hasa wale ambao hawajabarikiwa sana kimaisha. Namshukuru Mungu kwa upande wangu. unaposema kuongea namna hii nina shobo, unakuwa haueleweki and that defines what type of a man you are and paharps the level of life you belong. Mungu akusaidie.
 
yaani kila nikienda dodoma siishiwi kero. wakati mwingine watoza ushuru wao wa stand ya nanenane, wanakutozeni ushuru wa kuingia na gari, ticket unayo ila ukishushwa ukapande basi pale mlangoni uwe na ticket au hauna utatozwa tena. sasa huu ni wizi wa wazi kabisa, serikali imeishiwa hela namna hii hadi iwe inapora kwa wananchi?
Pole mkuu,uwe unasema unapokuja mkuu!Kwa Nini uteseke mwana JF wakati nipo Dodoma
 
Kiasi gani tukurudishie? Mtaacha ushamba lini?
in fact, hauna uwezo kunirudishia kitu, ila soon hao watu wako wataonyeshwa mfano, watakapojikuta wapo mikononi mwa TAKUKURU. mark my words.
 
Back
Top Bottom