Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke aache kutisha na kufedhehesha Waandishi wa Habari

Wacha wavune walichopanda.

Ilibidi toka kitambo wasuse kuzipa airtime taarifa za serikali wakati ule wanafungiwa fungiwa. Wangeheshimiwa.

Walizidi kulamba miguu ya serikali wakati ule wenzao wanafungiwa.
 
Ni aibu sana kwangu kuwa kabila moja na DED Mshamba kama huyu, aliyeletwa Temeke baada ya kuiba kura Kakonko.
 
Huyo Gondwe uliyempelekea kopi hana mamlaka yoyote kwa DED, mwenzake alifanikisha wizi wa kura Kakonko, sasa yeye ukabila tu ndio unambeba, atafanyaje?
 
Nahisi wewe ndiyo Ded mwenyewe
 
Mkuu,

Ni kweli majibu ya Mkurugenzi hayakuwa na hekima ya kiuongozi, sauti ilikuwa ni ya kutishia wakati akijua fika kabisa kuwa mwandishi katika utafutaji wake wa taarifa alikutana na wananchi hao ndipo wakaanza kutoa kero zao kwa manufaa ya umma. Mpaka hapo mwandishi hana kosa lolote, alichotakiwa kama hakupenda kutoa majibu kupitia simu angempangia siku mwandishi amfuate ofisini kwake ili apate ufafanuzi kutokana na sintofamu ya malalamiko ya wananchi kuliko kudai mwandishi huyo hana sifa ya kuongea naye labda amtaarifu Mkurugenzi wa chombo husika cha habari ampigie simu hizo ni dharau pamoja na kwamba wananchi wana hasira lakini pia ametengeneza hasira dhidi ya wamiliki wa vyombo vya habari.

USHAURI

Mamlaka husika (DC TEMEKE & MKUU WA MKOA DSM) imwonye huyo mkurugenzi na aombe radhi kwa kusababisha sintofamu kwenye jambo ambalo lilihitaji ufafanuzi tu ili mwandishi aiweke taarifa yake kwenye mizania sawia.

Mamlaka ya uteuzi (RAIS) Akishupaza shingo aondolewe kwenye nafasi hiyo maana hayupo kwa ajili ya kutatua kero za wananchi
 
Hayo majibu hutolewa na walio lewa madraka au alipigiwa simu akiwa katika hali ya msongo mawazo.

Yote kwa yote ni majibu ya kuudhi yasiyo stahili kutolewa na kiongozi au mtendaji wa shughuli kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania.
 
Aligombea Busokelo, siyo Rungwe. Wilaya ya Rungwe ina majimbo ya uchaguzi mawili: Busokelo (awali Rungwe Mashariki) na Rungwe (awali Rungwe Magharibi)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…