Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke aache kutisha na kufedhehesha Waandishi wa Habari

Walishindwa kitu gani hao wandishi kwwenda kwa Mkuu wa Wilaya ambaye ni Godwin Gondwe ambaye kimsingi ni Boss wake huyo DED angemlazimisha atoe majibu ya kueleweka ama angemalizana naye kisha yeye Gonmdwe alizungumzie hilo swala akiwa kama mwenye dhamana ya kila kitu kwwnye wilaya ikiwemo ulinzi na Usalama.

Viongozi wengi awamu hii ni wapuuzi sana kama mtu anamwambia mwenzie hana hadhi ya kuzungumza naye ina maana yeye anazungumza na malaika tupu ama? kwakweli tutaona mengi safari hii.
 
Yaani kwamba mtu akijenga jumba zuri mkoani ndio anakuwa hana njaa? Au mimi sijaelewa
Sio mkoan tu hata hapo dar haishi mwenye vibanda jamaa pesa ipo na sio ya kuunga unga.

Narudia Tena jamaa hana njaa Kama watu wanavyoongea hapa sema kakosea tu kuongea hivyo na ni hulka yake ila kusema ana njaaa hapana sio kweli hata akiachishwa leo ukurugenz narudia Tena hana njaa.
 
lakini kwa utaratibu walichofanya itv ni sahihi maana kiutaratibu mwenye majibu ni DED
 
Hizo pesa kazipata wapi? Maana inasemekana anahujumu miradi ya maendeleo kama mradi wa DMDP.
 
mzee unamsifia mwanaume mwenzako hata chawa hafikii huko....mwambie jamaa usilete utani kazini wamedondoshwa hadi mawaziri wakuu kitengo ni nani
Nimejibu hivyo kulinga na mmoja kudai ded ana njaa ,ndipo nikampa ukwel kuwa jamaa hana njaaa kabisa alaf unakuja kutukna hapa .

Au unadhan mm sijui kutukana
 
Sawa majibu anayo DED lakini kama yeye ni Mungu mtu unategemea nini lazima waende kwa bosi wake
huyu DED inasemekana hata baadhi ya viongozi wa mkoa na wilaya anawadharau nani yupo nyuma ya huyu jamaa?
 
Atajuta kwa nini alijibu hivyo, hana siku kwenye hy nafasi, hizi zama zingine, kajisahau.......
 
Atajuta kwa nini alijibu hivyo, hana siku kwenye hy nafasi, hizi zama zingine, kajisahau.......
Huyo hatoki leo Wala kesho yupo yupo sana bwasheee, yupo hapo kwa sabab maalum
 
Angekuwa hana njaa asingekuwa Temeke Bro, anasugua Goti, ana njaa kali na pasipo shaka utamsikia akiomba radhi kwa aliyomjibu mwandishi. Eti Hana njaa, wabongo bwana
 
mkurugenzi aliongea kwa madaha utadhani yuko kwenye kampuni yake binafsi
 
We unakaa tumboni kwake ndo umjue kwamba hana njaa?!
 
kutokuwa na njaa kwake ndio kuhalalishe kudharau waandishi? Kama mwandishi ambae anahitaji maelezo tu anajibiwa hivyo, je mwananchi mwenye shida atajibiwa nini?
Na hapo hakuna utani. Utani hufanywa kwa mtu unaemjua, mtu humjui utamtaniaje? Pia kwenye kazi huwa hakuna dhihaka. Huyo jamaa yako unaedai unamjua sana (kama sio wewe mwenyewe DED unajaribu kujisafisha) ni mlevi wa madaraka tu ambae keshajimithilisha na mungu mtu.
Sheria ya kwanza ya uongozi bora ni kumchukulia mfagiaji na meneja mkuu kwa heshima moja, sio kumpa mtu heshima kwa kulingana na hadhi yake.
 
Itoshe tu, kukumbusha kwamba wakurugenze, akiwepo Mwakabibi, walisimamia ‘jambo lile’ la October 28!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…