Mkurugenzi wa mashitaka,DPP, onekana kuwa upo.!

Mkurugenzi wa mashitaka,DPP, onekana kuwa upo.!

REAGAN C.MABOGO

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Posts
1,269
Reaction score
1,007
Imekuwa kana kwamba haupo kabisa! Au kana kwamba uliteuliwa ukiwa huna sifa! Mambo yafuatayo yanadhihirisha ninachokisema.: 1. Polisi baada ya kuwakamata watu kijinga kijinga, na kwa hoja za kijinga kijinga, cha ajabu imekuwa kana kwamba polisi ndiyo wanaamua kama mashitaka yafunguliwe ama la. Na hili ni pale sababu hizi za kijinga kijinga zinapozaa kesi za kijinga kijinga mahakamani (uchochezi) na kusababisha mzigo usio na maana kwa mahakama na mlundikano wa mahabusu magerezani.! 2. La pili ni la MAWAKILI KUUNGANISHWA KWENYE KESI ZA WATEJA WAO AU KUBAMBIKIWA KESI WAKIWA WAMEENDA POLISI KUWAONA WATEJA WAO.! Kwa njia ya kushitakiwa (MASHA na wengineo) NA kwa kuwekwa kwenye orodha ya mashahidi (KIBATALA).Na hasa hili la mawakili nilitegemea likushughulishe wewe kama mwanasheria. Lakini inasikitisha kuona kuwa umeamua kuwa sadaka na kubaki kutumiwa na makuhani madhabahuni. Huu ni udhaifu. Na Udhaifu wako ndiyo ulimfanya hata yule polisi anayejiita msangi kutamka bila aibu wala uoga kuwaunganisha mawakili .
 
Back
Top Bottom