Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Maswa (MAUWASA), Mhandisi Nandi Mathias James, amechukua rasmi fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania ubunge wa Jimbo la Buchosa, wilayani Sengerema, mkoa wa Mwanza.
Mhandisi Nandi(kulia)alikabidhiwa fomu hiyo leo, Juni 29, 2025, majira ya saa 8:30 mchana katika Ofisi za CCM Wilaya ya Sengerema mkoa wa Mwanza na Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Rashid Semendu.