Mkurugenzi wa Mawasiliano ameteuliwa lini?

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
Tulizoea sana kuona nafasi ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu ikitangazwa, taarifa pia zikiwekwa katika ukurasa wa Facebook wa Ikulu Mawasiliano na ukurasa wa Facebook wa Msemaji Mkuu wa Serikali.

Leo, Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imetiwa sahihi na Sharifa B. Nyanga kama Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu na si Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu kama ilivyokuwa siku za nyuma.

Hii inamaanisha Sharifa B. Nyanga ameteuliwa au amethibitishwa kuthibitishwa rasmi kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

Tunampongeza Sharifa B. Nyanga, tunaombea heri na baraka katika majukumu yake mapya.

Lakini swali linabaki kwa nini hawakutangaza uteuzi huo kama ilivyozoeleka. Lakini mazoea ni ndwele, ambayo haiponi bila kupata tiba. Sisi tuliozoea kuona tangazo la uteuzi tumeduwaa!

Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula.
Dar es Salaam, 30 Septemba 2024; saa 2:20 usiku
 
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 30 Septemba 2024; saa 2:20 usiku
Mbona juzikati tu ndani ya wiki mbili hizi.! Mambo mengine sijui mnakuwa mmefumba macho
 
Kwani yule tobias si ndo alikuwa mkurugenzi wa mawasiliano ikulu?
 
Back
Top Bottom