Mkurugenzi wa Moshi anafunga biashara zetu sababu ya kuchelewa kulipa kodi ya pango, hii ni sawa?

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
Halmashauri ya Manispaa ya Moshi imekuwa na tabia ya kutufungia maduka na biashara za Wafanyabiashara wa Stendi Kuu ya Mabasi kinyume na maelekezo ya Serikali yaliyotolewaa Julai 1, Mwaka 2023 na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alipokuwa Bungeni.

Mwigulu alisema ikiwa kuna changamoto za mlipo ya kodi na tozo nyingine za kibiashara hakutakiwi kufungwa bali inatakiwa kufanyike mazungumzo ili Mfanyabiashara ajue changamoto anayoipitia.

Kinachoendelea huku Moshi, Mkurugenzi wa Manispaa ndio anaongoza zoezi la fungafunga maduka hili si sawa.

Kama tunapata changamoto za kifedha, ukifunga biashara bila kutaka kusikiliza upande wetu unategemea sisi tutaishije?

Serikali kuu ingalie hii changamoto, Wafanyabiashara tunateseka, kwani kuna muda tunapata hasara, hivyo inakuwa ngumu kutimiza malengo ya kulipa malipo mbalimbali yanayotakiwa.

Hii fungia fungia imepitwa na wakati.



 
Mnataka haki, sawa. Mnatimiza wajibu wenu wa kulipa tozo, ushuru, leseni nk kwa wakati? Mkurugenzi anapimwa kazi yake kwa kuwabana mtekeleze wajibu wenu. Tatizo huja ikitajwa fedha tu. Hamtaki na mnapiga chenga kulipia mnachotakiwa kulipa. Lipeni muone kama huyo Mkurugenzi atafunga milango yenu ya biashara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…