Mkurugenzi wa NHIF: Aga Khan walisema huduma zao ni za viwango vya juu na bei tunazowalipa ni ndogo hivyo hawawezi kuendesha biashara

Mkurugenzi wa NHIF: Aga Khan walisema huduma zao ni za viwango vya juu na bei tunazowalipa ni ndogo hivyo hawawezi kuendesha biashara

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dkt. Irene Isaka, amesema mfuko huo unaendelea na mazungumzo na Hospitali ya Aga Khan ili kurejesha huduma za bima kwa wanachama wa NHIF katika kituo hicho jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya NHIF katika miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita, Dkt. Isaka alisema mazungumzo hayo yamefikia hatua nzuri.

Alifafanua kuwa sababu iliyosababisha Aga Khan kusitisha huduma za NHIF ni hospitali hiyo kujiona kuwa inatoa huduma za viwango vya juu ("high class"), hivyo haikuridhishwa na kiwango cha malipo kilichotolewa na NHIF kwa vifurushi vya bima.

"Kilichotokea ni kwamba wao wanasema huduma zao ni za viwango vya juu, na bei tunazowalipa ni ndogo, hivyo hawawezi kuendesha biashara," alisema Dkt. Isaka.

 
Kwa hiyo mfuko utafanyaje ili kumeet demand zao, watapewa upendeleo wa kuongezewa bei tofauti na vituo vingine au vipi?

Hili huenda linachangiwa na vigogo serikalini ambao hawataki kutibiwa kwenye hospital zetu hizi wanataka watibiwe huko Agakhan na withdraw ya mfuko kwenye hiyo hospital kunawaumiza maana hawawezi kupata huduma huko kwa sasa
 
Back
Top Bottom