- Ni lazima kutoa credit inapokuwa due, hapa ninampa rais Kikwete heshima kubwa sana. Hapa JF ndipo ukweli wa ufisadi wa Richimonduli ulipoanzia kufichuliwa rasmi, na kuna tuliolala macho kulifanyia kazi taifa letu, sasa matokeo ndio haya yameanza kuonekana,
- Tumesikia mengi sana kuhusiana na nguvu walizonazo mafisadi katika taifa letu hasa wa Richimonduli, na kama kawaida hapa ya JF wananchi karibu wote hapa tunashuhudia one of the untouchables akifungua njia ya Kisutu, lakini kama kawaida kuna ma-intellectuals tayari wanaotaka kutuambia kua sio kweli tunayoyaona na kwamba eti Richimonduli itaishia na huyu Msomali tu, hivi mbona jana na juzi hamkutuambia kuwa leo kuna Msomali atatinga since mnaonekana kujua sana kinachoendelea kuliko hata serikali yenyewe? Eti mlijua lini kuwa serikali itamfikisha Msomali tu kuhusiana na Richimonduli? Mbona hamkutuambia mapema?
- I mean wananchi tunaona mbili, wengine mnatuambia ni tatu sasa tuambieni basi kesho ni zamu ya nani? au who is next? Yaani rais na serikali yake anaweza kuwa mjinga kiasi gani hasa cha kudiriki kumpeleka Msomali bila washirki wake?
Ninampongeza rais wa jamhuri kwa hili la kumfikisha huyu fisadi la Richimonduli kwenye sheria, na ninaamini kuwa wengine wote wako njiani, yaani kuanzia Mary Kejo, Msabaha, Karamagi, Lowassa, Rostam, Manji, Mwakapugi, na wengineo, tunaamini kwamba huyu Msomali ni mwanzo tu! Hapa Muheshimiwa sana Rais tuko pamoja, na Mungu Akubariki, lakini tunasubiri na wengine pia.
Mungu Aibariki Tanzania!