Mkurugenzi wa TANESCO Felchesmi Mramba: Tanzania kuuza umeme nje ya nchi mwaka 2016

idoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2013
Posts
3,051
Reaction score
1,416
Tanzania inakusudia kuzalisha umeme wa kutosheleza mahitaji ya Watanzania wote na ziada kwa ajili ya kuunza nje ya nchi ifikapo mwaka 2016.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Felchesmi Mramba, aliyasema hayo wakati wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Wafanyakazi wa shirika hilo nchini unaofanyika kwa siku mbili jijini Mbeya.

Alisema kuwa Tanesco imeanza ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi katika eneo la Kinyerezi, Dar es Salaam kwa ajili ya kuzalisha umeme wa kutosheleza mahitaji ya nchi pamoja na ziada.

Alisema tayari awamu ya kwanza na ya pili ya mradi huo (Kinyerezi One na Two) yenye uwezo wa kuzalisha jumla ya megawati 350 za umeme, imekamilika kwa asilimia 90 na inatarajiwa kuanza kazi ifikapo Machi, mwakani.

Alisema awamu ya tatu na ya nne zitajengwa kwa ubia na Kampuni ya Kichina, ambapo katika awamu ya tatu Kampuni ya Kichina itamiliki asilimia 60 ya hisa na Tanesco itamiliki asilimia 40, huku awamu ya nne ambayo itakuwa na mtambo wa kuzalisha megawati 600 za umeme, Tanesco itam6iliki asilimia 30 na kampuni ya Kichina itamiliki asilimia 70.

Kwa mujibu wa Mramba, miradi hiyo yote itarajiwa kukamilika na kuanza kufanya kazi ifikapo mwaka 2016, hali ambayo italifanya tatizo la kukatika katika kwa umeme nchini kubaki historia.

Alisema katika mikakati ya kuuza ziada ya umeme nje ya nchi, tayari Tanesco imesaini mkataba wa kujenga njia kubwa ya kusambaza umeme kwa nchi tatu za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kuuziana umeme wa ziada.

Alisema sehemu ya kwanza ya ujenzi wa njia hiyo itakuwa ni kuanzia Nairobi nchini Kenya hadi Singida na awamu ya pili itaanzia Iringa kuelekea Dodoma, njia ambayo itaendelezwa hadi mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Hata hivyo, wakati shirika hilo likitangaza mikakati hiyo mizuri yenye matumaini kwa Watanzania, mgeni rasmi kwenye mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, kupitia katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Profesa Norman Sigalla, alisema kuwa Tanesco haitaeleweka kirahisi kwa wananchi kama mikakati hiyo haitatekelezwa kwa vitendo.

Source: Nipashe
 
Mmh..nje ya nchi wakati kuna WATANZANIA ngorongoro hakuna umeme...na nauhakika hadi hiyo 2016 watakuwa hawana umeme kwan ad now amna harakati zozote za kuanza japo hata.....mikakati ya kuwasambazia
 
Tanesco ni very hopeless, hapa ninapoandika sredi hii hatuna umeme tokea saa mbili asubuhi. Pia jana hatukuwa na umeme tokea saa 12 jioni hadi saa 6 usiku. Huyu mkurugenzi anaropoka kama Nape Nauye, na si rahisi kutofautisha kati ya wawili hawa. Miaka kibao wimbo ni ule ule. Ukikata umeme si kwamba unamkomoa mtumiaji pekee bali pia shirika linapata hasara kubwa maana wakati inapotakiwa kuuza weww bidhaa ya kuuza huna. Sijui hawa viongozi wa tanesco ni mburula kabisa logic rahisi kama hii inawashinda?

Hayo mawazo ya kuuza umeme nje ya nchi ni rhethorics na wala hakuna facts wala ueledi katika kauli hiyo. Very hopeless
 
Tanzania inakusudia kuzalisha umeme wa kutosheleza mahitaji ya Watanzania wote na ziada kwa ajili ya kuunza nje ya nchi ifikapo mwaka 2016.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Felchesmi Mramba, aliyasema hayo wakati wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Wafanyakazi wa shirika hilo nchini unaofanyika kwa siku mbili jijini Mbeya.

Alisema kuwa Tanesco imeanza ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi katika eneo la Kinyerezi, Dar es Salaam kwa ajili ya kuzalisha umeme wa kutosheleza mahitaji ya nchi pamoja na ziada.

Alisema tayari awamu ya kwanza na ya pili ya mradi huo (Kinyerezi One na Two) yenye uwezo wa kuzalisha jumla ya megawati
350 za umeme, imekamilika kwa asilimia 90 na inatarajiwa kuanza kazi ifikapo Machi, mwakani.

Alisema awamu ya tatu na ya nne zitajengwa kwa ubia na Kampuni ya Kichina, ambapo katika awamu ya tatu Kampuni ya Kichina itamiliki asilimia 60 ya hisa na Tanesco itamiliki asilimia 40, huku awamu ya nne ambayo itakuwa na mtambo wa kuzalisha megawati 600 za umeme, Tanesco itam6iliki asilimia 30 na kampuni ya Kichina itamiliki asilimia 70.

Kwa mujibu wa Mramba, miradi hiyo yote itarajiwa kukamilika na kuanza kufanya kazi ifikapo mwaka 2016, hali ambayo italifanya tatizo la
kukatika katika kwa umeme nchini kubaki historia.

Alisema katika mikakati ya kuuza ziada ya umeme nje ya nchi, tayari Tanesco imesaini mkataba wa kujenga njia kubwa ya kusambaza umeme kwa nchi tatu za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kuuziana umeme wa ziada.

Alisema sehemu ya kwanza ya ujenzi wa njia hiyo itakuwa ni kuanzia Nairobi nchini Kenya hadi Singida na awamu ya pili itaanzia Iringa kuelekea Dodoma, njia ambayo itaendelezwa hadi mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Hata hivyo, wakati shirika hilo likitangaza mikakati hiyo mizuri yenye matumaini kwa Watanzania, mgeni rasmi kwenye mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, kupitia katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Profesa Norman Sigalla, alisema kuwa Tanesco haitaeleweka kirahisi kwa wananchi kama mikakati hiyo haitatekelezwa kwa vitendo.

CHANZO: NIPASHE

Hapo kwenye red mashaka matupu. Hilo neno la 'historia' limeshasemwa na viongozi mara nyingi sana ikiwa ni pamoja na waziri Pinda mwaka 2011 wakati ukijengwa mtambo pale Ubungo Megawati 100 na tunashuhudia kuwa hakuna mabadiliko yoyote.
 
Kwanini wasinyamaze kimya tukaona vitendo. Waache kuwa na sifa za kilevi.
 
Hapo kwenye red mashaka matupu. Hilo neno la 'historia' limeshasemwa na viongozi mara nyingi sana ikiwa ni pamoja na waziri Pinda mwaka 2011 wakati ukijengwa mtambo pale Ubungo Megawati 100 na tunashuhudia kuwa hakuna mabadiliko yoyote.

Mie niliisikia hii mwaka 2007 toka kwa Le Professer mwenyewe huku pembeni akiwa na Ngeleja.. Alisema mgao ungekuwa historia.. Well mpaka leo umegoma kuwa historia wala jiografia..
 
Huyu Mramba anaanza kuleta habari za bosi wake Muhongo!!sijui nae anajiandaa kugombea Ubunge?
 
Walipoanzisha IPTL walituambia mgao utakuwa historia, walikuja netgroup solution walituambia mgao utakuwa historia, Richmond hivyo hivyo, songas, Aggrecco hivyohivyo na sasa Bomba la gesi toka mtwara na mitambo ya kinyerezi. Wataaminika vipi? historia imebaki kuwa historia.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Tanzania inakusudia kuzalisha umeme wa kutosheleza mahitaji ya Watanzania wote na ziada kwa ajili ya kuunza nje ya nchi ifikapo mwaka 2016.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Felchesmi Mramba, aliyasema hayo wakati wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Wafanyakazi wa shirika hilo nchini unaofanyika kwa siku mbili jijini Mbeya.

Alisema kuwa Tanesco imeanza ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi katika eneo la Kinyerezi, Dar es Salaam kwa ajili ya kuzalisha umeme wa kutosheleza mahitaji ya nchi pamoja na ziada.

Alisema tayari awamu ya kwanza na ya pili ya mradi huo (Kinyerezi One na Two) yenye uwezo wa kuzalisha jumla ya megawati 350 za umeme, imekamilika kwa asilimia 90 na inatarajiwa kuanza kazi ifikapo Machi, mwakani.

Alisema awamu ya tatu na ya nne zitajengwa kwa ubia na Kampuni ya Kichina, ambapo katika awamu ya tatu Kampuni ya Kichina itamiliki asilimia 60 ya hisa na Tanesco itamiliki asilimia 40, huku awamu ya nne ambayo itakuwa na mtambo wa kuzalisha megawati 600 za umeme, Tanesco itam6iliki asilimia 30 na kampuni ya Kichina itamiliki asilimia 70.

Kwa mujibu wa Mramba, miradi hiyo yote itarajiwa kukamilika na kuanza kufanya kazi ifikapo mwaka 2016, hali ambayo italifanya tatizo la kukatika katika kwa umeme nchini kubaki historia.

Alisema katika mikakati ya kuuza ziada ya umeme nje ya nchi, tayari Tanesco imesaini mkataba wa kujenga njia kubwa ya kusambaza umeme kwa nchi tatu za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kuuziana umeme wa ziada.

Alisema sehemu ya kwanza ya ujenzi wa njia hiyo itakuwa ni kuanzia Nairobi nchini Kenya hadi Singida na awamu ya pili itaanzia Iringa kuelekea Dodoma, njia ambayo itaendelezwa hadi mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Hata hivyo, wakati shirika hilo likitangaza mikakati hiyo mizuri yenye matumaini kwa Watanzania, mgeni rasmi kwenye mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, kupitia katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Profesa Norman Sigalla, alisema kuwa Tanesco haitaeleweka kirahisi kwa wananchi kama mikakati hiyo haitatekelezwa kwa vitendo.
CHANZO: NIPASHE
🙆🙆🙆🙆🙆🙆🙆😀
 
Back
Top Bottom