Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Ramadhan Kailima ametoa wito kwa wananchi kujitokeza na kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura awamu ya Pili, ambapo tayari zoezi hizo limeanza katika baadhi ya mikoa nchini.
Akizungumza mkoani Tabora, Kailima amesema kwa sasa daftari hilo lipo wazi, hivyo wananchi wajitokeze kuhakiki taarifa zao ili kama kuna kasoro kuzirekebishwe mapema kabla ya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.