Mkurugenzi wa upepelezi wa Makosa ya jinai (DCI Robert Manumba) astaafu ...!!

Mkurugenzi wa upepelezi wa Makosa ya jinai (DCI Robert Manumba) astaafu ...!!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Mkurugenzi wa upepelezi wa Makosa ya jinai (DCI Robert Manumba) astaafu ...!!







Jeshi la Polisi nchini linapenda kuutaarifu umma kwamba aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya jinai (DCI) Robert Manumba amefikia umri wa kustaafu kisheria ambao ni miaka sitini (60) katika utendani wake wa kazi.


Aidha, katika utumishi wake ndani ya Jeshi la Polisi amefanya kazi katika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Chumba cha kupokea mashtaka kuanzia mwaka (1976 – 1977), mwendesha mashtaka

wilaya ya Kibondo na Kasulu mkoani Kigoma, 1977 – 1984), Mkufunzi katika chuo cha polisi Dar es salaam, (1984 – 1987), Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Magomeni na Kinondoni na Naibu Mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Dar es salaam (1987 – 1993),

Pia, amewahi kuwa Mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Arusha, ( 1993 – 1995), Mkufunzi mkuu wa Chuo Cha Polisi Moshi ( 1995 – 1996), Mkuu wa kitengo cha Fraud makao makuu ya upelelezi,

(1996 – 1997), Mkuu wa kitengo cha usalama wa nchi, intelijensia na madawa ya kulevya makao makuu ya upelelezi (1997 – 2001) na kuwa msaidizi wa mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini (2001 – 2006). Kuanzia mwaka 2006 hadi anastaafu, alikua Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini.

Aidha, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema, amemshukuru na kumpongeza (DCI) Manumba anayestaafu kwa kulitumikia taifa katika nyadhifa mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi kwa

weledi na uwaminifu mkubwa wakati wote alipokuwa mtumishi ndani ya Jeshi la Polisi.

Pia, amemtaka kuendelea kuwa msaada kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa ushirikiano wa namna yoyote ile unaoweza kusaidia kupunguza uhalifu hapa nchini kwasababu suala la usalama ni

taaluma kama zilivyo taaluma zingine, na taaluma hiyo wanayo watu wachache.

Hata hivyo, wakati tataratibu wa uteuzi wa mkurugenzi wa upulelezi ukiendelea, mkuu wa ufuatiliaji na tathimini CID makao makuu, kamishina Isaya Mungulu, atakua akikaimu nafasi hiyo

Mkurugenzi wa upepelezi wa Makosa ya jinai ( DCI Robert Manumba ) astaafu ...Mungulu ateuliwa kukaimu kwa muda. - MPEKUZI

 
Astaafu tu..kwanza ndo vizuri ili apate muda wa kuhudumia mwili wake.,,, ..
 
Hongera kwa kumaliza salama, idara yako ndio mhimili mkuu wa ukachero katika jeshi la polisi, subiri another post kama adadi rajabu
 
aondoke tupate damu mpya itakayo weza kukabiliana na changamoto tulizo nazo ktk nchi yetu kwa kipindi hiki.
Uhalifu bado upo kwa kiwango cha juu sana.
 
Back
Top Bottom