Mkurugenzi wa VODACOM, TIGO, ZANTEL, TTCL, AIRTEL pitieni hapa, huwenda kukawa kuna faida kwenu

hiyo njia ni ndefu, pia itahitaji mpesa wapate commission.

Kuibiwa hakuwezi kwepeka. inategemea na inteligensia ya muuzaji na mnunuaji.

kitu ninachokiona ni kibaya ni pale unauza kitu, unatumiwa muamala feki au unatumiwa pesa inaingia halafu mtu anapiga simu kuomba irudishwe as if amekosea muamala.

cha kufanya ni issue moja.

Muuzaji awe na uwezo wa kutengeneza quote. ambayo ina maelezo na bei ya huduma au bidhaa inayouzwa na kisha kisha mlipaji atapewa quote ya namba kisha itakuwa reference wakati analipa pesa.

So hapa tutaepuka miamala feki ike inayokujaga na Msg ya Mpesa/ Tigopesa pia pesa ikiingia kwenye hiyo quote, mnunuaji hawezi reverse muamala mpaka makubaliano maalum
 
Safari on Kenya wana hii kitu
 
Wazo zuri...ila badi halijakidhi haja 100% ya lengo tarajiwa.

1. Vipi pale mnunuzi anapokuwa hana uamjnifu na hatumi hizo namba za uthibitisho kwa muuzaji baada ya kupokea bidhaa??

2. Mtandao wa simu unakuwa na uthibitisho gani wa kuwa bidhaa imefika au haijafika pale mnunuzi unapoamua kutotuma code ya uthibitisho ??

3. Mitandao ya simu inakuwa inabeba dhamana ya mtu wa kati kati..Je,wanafaidikaje na muamala huu ukiacha ada za kawaida za utumaji na kupokea ??
 
wazo zuri ila halitekelezeki sababu kuna mambo yanafanyika nje ya mfumo na inahitaji tena uaminifu wa muuzaji na mnunuzi kukamilisha, chukua mfano wa aliexpress ukilipia kitu pesa wanakaa nayo wao mzigo ukifika seller ndio analipwa hii njia kwao inawezekana sababu wana tracking system ya kujua mzigo ulipo toka umetumwa.
Njia rahis ini kumtuma mtu aukague mzigo kabla hujanunua au tuwe na mfuoma kama wa amazoni au aliepress katika kufanya manunuzi.
 
Bado bado bado sana, una wazo zuri sana lakini bado wazo lako haliwezi kufanya kazi kwa ufanisi.

Mfano, kuna ile ukienda kutoa pesa kwenye ATM huwezi kuchukua pesa kama hujatoa kadi, post n kwann.? Watz sisi tukishapata tunachokihitaji hatuwezi kumkumbuka aliyetusaidia, vp kama nimepata mzigo lkn sijathibitisha.?

Nadhani tuendelee hv hv na ibaki kuwa na uaminifu kati ya muuzaji na mnunuzi.
 

Kwa namna hii voda watashikilia pesa hadi wachokee na itawalazimu wawe na mahakama yao
 
Hakika wazo ni zuri lakini bado kuna maeneo ya muhimu hayajatatuliwa.

1. Umesema mnunuzi hawezi kurudisha fedha baada ya kulipa..Sasa je,akiletewa bidhaa ambayo siyo ya vigezo vyake inakuwaje ??

Nadhani ili huu mfumo ufanye kazi lazima kuwe na self reversal (Mnunuzi kueeza kurudisha fedha zake pale ambapo bidhaa inakiwa tofauti na alichoagiza).

2. Kwa mitandao ya simu,hii ni huduma ya nyongeza (add on) hivyo ni lazima gharama za ziada ziwepo.Kazi ya kuwa verifier au middleman ni risk na lazima mitandao itranslate risk hii kwa malipo.
 
We jamaa una akili sana Mungu akubariki
 
1. Inawezekana, ila kwa due process ama due diligence; siyo mnunuzi kujiamulia kuichunia ilhali amepokea bidhaa ama muuzaji kama amedanganya.

2. Makato ni yaleyale ya kawaida na mitandao itafaidikia hapo, sana tu. Business "itachanganya" na wateja wengi, kama si wote, watatokea kuamini katika usalama wa mitandao 100%.
 
34h3h45
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…