Mkurugenzi ZBC atembelea Ubalozi wa Tanzania Comoro

Mkurugenzi ZBC atembelea Ubalozi wa Tanzania Comoro

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
IMG-20241114-WA0036.jpg

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Ramadhani Bukini leo ametembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro ambapo amefanya mazungumzo na Maafisa Ubalozini hapo wakiongozwa na Mhe. Balozi Saidi Yakubu.

Bwana Bukini alitumia wasaa huo kuelezea maboresho yanayoendelea katika ZBC na namna katika miaka minne ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi mambo yalivyoimarika ikiwemo kuwemo katika mitandao ya kijamii, kupata vifaa vya kisasa na kufikia watazamaji wengi zaidi na pia kuwa na mkakati wa kuliendesha Shirika hilo kibiashara jambo linaloenda vyema mpaka sasa.

IMG-20241114-WA0038.jpg

Bwana Bukini alikuwa nchini Comoro ikiwa ni utekelezaji wa Mkataba wa Ushirikiano baina ya ZBC na Shirika la Utangazaji la Comoro (ORTC).

IMG-20241114-WA0042.jpg
 

Attachments

  • IMG-20241114-WA0044.jpg
    IMG-20241114-WA0044.jpg
    1 MB · Views: 1
Back
Top Bottom