Mkutano katika Sekta ya Afya

Mkutano katika Sekta ya Afya

iamwangdamin

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2015
Posts
864
Reaction score
1,798
Tarehe 31 Julai 2024 kuanzia saa 5 asubuhi utafanyika mkutano baina ya Taasisi zinazoshughulika na tafiti za afya nchini Tanzania na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Afya ya nchini Uingereza (National Institute for Health and Care Research (NIHR).

Mkutano huo umeandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza kwa madhumuni ya kuwezesha taasisi za Tanzania kupata ufahamu juu ya fursa za ushirikiano na ufadhili wa shughuli za utafiti katika sekta ya afya.

Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na taasisi mbalimbali nchini ikiwemo taasisi ya @NIMR_Tanzania; @ifakarahealth, @muhimbiliuniver, @kcmucotz, @cuhas_bugando, @hkmuniversity, @MuhimbiliOrtho1, @TaasisiMoyoJKCI, @MuhimbiliTaifa, UDOM, Hospitali ya Benjamin Mkapa na Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.

Mkutano huo utafanyika chini ya wenyeviti wenza Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Ndugu @MbelwaK na Mkurugenzi wa Afya wa NHRI Profesa Kara Hanson. Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu atahudhuria Mkutano huo.

iamwangdamin
 

Attachments

  • 20240729_173733.jpg
    20240729_173733.jpg
    48.3 KB · Views: 5
  • 20240729_173731.jpg
    20240729_173731.jpg
    65.7 KB · Views: 4
  • 20240729_173728.jpg
    20240729_173728.jpg
    7.5 KB · Views: 4
Back
Top Bottom