Pre GE2025 Mkutano mkubwa wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Nchimbi

Pre GE2025 Mkutano mkubwa wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Nchimbi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi leo alasiri anatarajiwa kuzungumza na wananchi wa Lindi kwenye mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika Uwanja wa Mpilipili, Mjini Lindi.

Balozi Nchimbi na msafara wake, atapokelewa rasmi katika Ofisi za CCM za Mkoa huo, ambapo atafanya kikao na Kamati ya siasa na baadaye mkutano wa ndani wa makundi mbalimbali.

Lengo la ziara hiyo ni; Kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020, kuhuisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki Taarifa zao na kujiandikisha katika Daftari la Wapiga kura, kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Novemba mwaka huu.

Katika ziara hii Dk Nchimbi kabla ya kuingia mkoani Lindi, amemaliza ziara ya siku mbili mkoani Mtwara, ambapo ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amosi Makalla, Katibu wa NEC-Organaizesheni Ndg. Issa Ussi Haji (Gavu) pamoja na Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Rabia Abdallah Hamid.

20240730_124818.jpg
 
Back
Top Bottom