Tunaomba wanasheria wa CCM watufafanulie hapa
Kwa Mujibu wa Katiba ya CCM, Toleo la Mwaka 2012 Ibara ya (105), Inazungumzia Kazi za Mkutano Mkuu. Ibara Ndogo ya (03), ya Ibara ya (105), ya Katiba ya CCM toleo la Mwaka 2012 inaipa Mkutano Mkuu mamlaka ya Kuthibitisha, Kubadili, kukataa, au kuvunja uamuzi wowote uliotolewa na kikao chochote cha chini yake au na yeyote wa CCM. Mkutano Mkuu ndio Ngazi ya Juu na ya Mwisho ya Kimaamuzi ndani ya CCM kwa mujibu wa Ibara ya (104), Ibara Ndogo ya (2), ya Katiba ya CCM,
Au ndo goli la Mkono?