Doctor Mama Amon
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 2,089
- 2,725
Mhe. Tundu Antipas Mughway Lissu, Mwenyekiti Mtarajiwa wa Chadema na Mgombea Urais Mtarajiwa Katika Uchaguzi wa 2025
Kutokana na mikutano mikuu ya Chadema na CCM inayofanyika kwa kufuatana ndani ya Januari 2025 sasa ni wazi kwamba busara kongwe za wanazuoni zitaanza kutimia.
Wanazuoni wengi husema kwamba ukweli uliochujwa hupatikana kutokana na mchakato wa mnyukano wenye hatua tatu zinazojumuisha mapendekezo, mapingamizi, mikingamo na majumuisho.
Katika hatua ya kwanza kuna mnyukano kati ya mapendekezo yenye kusindikizwa na ushahidi wa daraja la kwanza, daraja la pili, na daraja la tatu, na mapingamizi dhidi ya yote haya (claims vs objections)
Katika hatua ya pili kuna mchakato wa mnyukano kati ya mapingamizi na mikingamo dhidi ya mapingamizi (objections vs rebuttals)
Na katika hatua ya tatu mchakato huu huzalisha hitimisho la ukweli uliochujwa ambao ni zao la upatanisho wa kimaarifa lenye kusuluhisha mnyukano kati ya mapendekezo, mapingamizi na mikingamo (qualified conclusion)
Busara hizi zitaaanza kutimia machoni mwa wapiga kura wa Tanzania kuanzia kesho baada ya uchaguzi mkuu wa Chadema.
Uchaguzi huu wa Chadema utaweza kutoa mapingamizi dhidi ya mapendekezo ya CCM.
Kisha CCM wataleta mikingamo dhidi ya mapingamizi ya Chadema.
Sisi wapiga kura tutakuwa watazamaji katika mnyukano huu.
Hatimaye tutatoa suluhisho kupitia sanduku la kura.
Ni katika muktadha huu, taarifa zimelifikia dawati la utafiti la Dkt Mama Amon zikionyesha kuwa kesho huenda Mkutano Mkuu Chadema ukajibu Mapigo dhidi ya mkutano wa CCM uliofanyika jana.
Jana huko Dodoma, wajumbe wa CCM walitumia kanuni ya "early timer politics" kumteua Makamu Mwenyekiti wa CCM, Mgombea Urais wa CCM, na Mgombea Mwenza wa CCM katika nafasi ya Urais, ifikapo Oktoba mwaka 2025.
Kwa kufuata mantiki ile ile ya "kunywa supu ikiwa bado ya moto," inaelekea kwamba, sasa Chadema nao watajibu mapigo ili kuimarisha midahalo ya kusiasa kuelekea 2025.
Na uwezekano mkubwa ni mwamba Tundu Antipa Mughwai Lissu atasimikwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa Chadema Taifa kwa kura zaidi ya 50%, atatangazwa Mgombea Urais 2025, na pia Mgombea Mwenza wake atatajwa.
Wote hawa watathibitishwa na Mkutano Mkuu wa Chadema.
Ni mtindo wa bandika bandua, piga nikupige, kunywa chai kabla haijapoa.
Kwa kuzingatia ukuu wa haki ya kikatiba ya kila raia anayetaka kugombea na kuchaguliwa katika nafasi yoyote ya uongozi, kama isemavyo ibara ya 21 ya Katiba ya Tanzania (1977), mpaka sasa watu wafuatao wanatajwa kuwa na nafasi kubwa ya kusimikwa katika nafasi ya Mgombea Mwenza wa Lissu:
Wakili Fatuma Karume, Prof. Assad, Mohammed Gassany, Wakili Mwabukusi, Wakili KIbatala, Dkt Bagonza, Dkt Slaa na watu eengine kadhaa
Fatuma karume
Professa Assad
Mohamed Ghassany
Wakili Mwabukusi
Peter KIbatala
Ask. Dkt. Benson Bagonza
Balozi Dkt. Wilbrod Slaa
Hebu tujiulize maswali machache:
Unadhani mgombea urais kwa tiketi ya Chadema atakuwa nani?
Kama ni Lissu Unajua Mgombea mwenza wa Lissu atakuwa nani?
Unafikiri kujulikana kwa Mgombea Urais wa Chadema na Mgombea mwenza wake kutakuwa na mchango kiasi gani katika kuchangamsha pilika za siasa za Tanzania?
Unadhani kati ya Timu CCM na Timu Chadema ni timu gani yenye mikakati iliyo na zindiko kubwa dhidi ya mishale ya kambi hasimu?
Na je, kati ya Timu Chadema na Timu CCM, unadhani ni timu gani itakuwa na mguso wa karibu kwa wapiga kura wa Tanzania ya leo?
Uhakika ni kwamba yaliyotokea kwenye Mkutano wa CCM Dodoma jana yamefungua ukurasa mpya katika siasa za Tanzania, yakiwa yanatuonyesha ukweli-nusu.
Tayari tunajua "Kisigino gani chenye udhaifu wa zindiko katika mikakati ya CCM," yaani "CCM's Achilles' Heel"
Lakini, yajayo kutoka Dar Es Salaam kwenye Mkutano Mkuu wa Chadema yatatoa sura kamili ya siasa za Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.
Yaani tutaweza kufahamu "Kisigino gani chenye Udhaifu wa zindiko katika mikakati ya Chadema," yaani "Chadema's Achilles' Heel."
Ni baada ya hapo, bila kupiga ramli tutaweza kuwatangazia Watanzania mshindi wa uchaguzi wa Urais ifikapo Oktoba 2025 atakuwa ni nani hasa!
Hao Watanganyika kina Wakili Mwabukusi, Wakili Kibatala, Aslofu Dkt Bagonza, Dkt. Slaa na watu baki kama wao, wanatajwa kwa sababu moja ya kikatiba.
Kwa mujibu wa ibara ya 21 ya Katiba ya Tanzania (1977) wao ni raia wenye haki ya kugombea na kuchaguliwa katika nafasi yoyote ya uongozi wa nchi.
Kwa sababu ya kifungu hiki l wigo wa kijiografia wa wagombea wa nafasi ya Umakamu Rais wa Tanzania unagusa kona zote za Tanzania ukiwemo upande wa Tanganyika na Zanzibar bila kujali mgombea urais wa Tanzania ametoka wapi.
Kwa mtazamo wa kisheria, hii maana yake ni kwamba, kifungu cha 47(3) cha Katiba ya Tanzania (1977) ni ubatili na utupu tangu mwanzo.
Yaani kifungu hiki cha 47(3) ni ubatili na utupu tangu mwanzo. Yaani, NULL AND VOID AB INITIO.
Ubatili wake unatokana na ukweli kuwa kinabagua kimakosa baadhi ya Watanzania, ambao kwa mujibu wa ibara ya 21 ya Katiba hiyo hiyo, wanayo haki, na wanataka kugombea nafasi ya Umakamu wa Rais wa Tanzania.
Kifungu hiki batili kinasomeka kama ifuatavyo:
"47(3) Mtu atateuliwa kugombea kiti cha Makamu wa Rais kwa kufuata kanuni kwamba endapo Rais wa Jamhuri ya Muungano atatoka sehemu moja ya Muungano, basi Makamu wa Rais atakuwa ni mtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano."
Inasemekana kuwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema wameapa kutotanbua uhalali wa kifungu hiki cha kikatiba kwa sababu iliyotajwa hapo juu.
Sasa, baada ya kusema hayo, na kabla ya kumalizia niseme neno kuhusu dhana ya "Kisigino chenye udhaifu wa zindiko katika mikakati ya kina Achilles."
Kulingana na Ngano za kale za Wagriki, "Kisigino chenye udhaifu wa zindiko katika mikakati ya Achilles" ni maneno yanayomaanisha udhaifu wa mtu mwente maguvu ukiwa umefichika mwilini mwake, kiasi kwamba, adui yake akiufahamu na akajipanga kushambulia vizuri eneo la mwili wake lisilo na zindiko, basi adui anapata ushindi kamili.
Katika Ngano za kale za Wagriki, mama yake Achilless alimtosa mtoto wake kwenye mto ulioitwa "Styx" ili kumpa zindiko la kimwili litakalomlinda na mabaya ya dunia hii.
Wakati mama anamzamisha Achilles kwenye mto huo alikuwa ameshika kisigino cha mguu wa kulia cha mtoto huyo.
Hivyo, kisigino hicho cha kulia hakikuzamishwa kwenye maji ya mto na hivyo hakikupata zindiko kabisa.
Baadaye, Achilles alikua na kuwa askari hodari aliyefanikiwa kubutua mishale na risasi zote kwa sababu mwili wake wote ulikuwa na zindiko maalum likinfanya aonekane kama mtu aliyevakia jaketi la kuzyia risasi yaani bullet proof coat.
Lakini, siku moja akiwa katika vita ya "Trojan" maadui zake walipata kujua siri kuhusu kisigino gani cha Achilles hakina zindiko kabisa.
Hivyo walifyatua mishale yenye sumu kukilenga kisigino kile, cha kulia, na hatimaye mshale mmoja ukamchoma na kuondoa uhai wa jasiri Achilles.
Tangu wakati huo, maneno "Kisigino cha udhaifu wa zindiko katika mikakati ya Achilles" hutumika kumaanisha kipengele cha udhaifu wa mtu, mfumo, taasisi au mikakati.
Tayari tunajua kisigino cha udhaifu wa zindiko la mikakati ya Timu CCM ni kipi.
Kesho tutajua vema kisigino cha udhaifu wa zindiko la mikakati ya Timu Chadema ni kipi.
Stay tuned.
=========UPDATES=========
A. MATOKEO YA MWENYEKITI TAIFA
- Odero Odero - Kura 01 Sawa na 0.1%
- Freeman Mbowe - Kura 482 Sawa na 48.3%
- Tundu Lissu - Kura 513 Sawa na 51.5%
B. MATOKEO YA MAKAMU MWENYEKITI BARA
- Mathayo Gekul - Kura 49 Sawa na 5%
- Ezekia Wenje -Kura 372 Sawa na 37%
- John Heche - Kura 577 Sawa na 57%
- Uamuzi wa chama ni kwamba watavuka mto baada ya kuufikia. Kwa sasa kipaumbele sio uchaguzi bali mageuzi ya kimfumo kwa ajili ya kuweka uwanja wa uchaguzu ulio tambarare kwa washirikibwote. Video ifuatayo inafafanua;
View attachment 3210255