Mkutano Mkuu wa Klabu ya Simba SC, MO kupewa timu leo

Wana simba watafanya kosa kubwa kutokumoa MO club , hawa wanaojiita wazee wa simba na wanachama hawajui usajili unafanyika kwa pesa za nani, hawajui makocha na wachezaji wanalipwaje wao kutwa nzima ni kuleta fujo na vurugu pale timu inapofanya vibaya. Nilimsikia mzee Fulani cjui kolomoni anaongea utumbo tu. Wale ni wazee wasio na kazi kutwa nzima ukienda pale msimbazi au jangwani Asubuhi unawakuta wanazozana hawataki kifanya kazi. Acha Mo apewe timu nchi ipige hatua. Hata sana wanga waanze kufikiria kumpa Manji timu akimaliza matatizo yake. Wanachama uchwara wamepitwa na wakati

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania kamwe hatutapata mafanikio ya mpira wa miguu bila kufanya mabadiliko ya umiliki na uendeshaji wa vilabu vyetu,Simba mpeni hisa Mo, hao watakaobaki na mifumo ya kizamani ya uendeshaji timu wataona mfano, kuwa kama Tp Mazembe, Al Ahly, Zamalek hakuwezi kutokea kama miujiza, sie mashabiki tunataka raha tu, nani anamiliki timu sio issue kwetu.
 
Yanga washachelewa kwa Manji...bahati haiji Mara 2: Simba wakichemka hapa, wasitafute mchawi mbeleni. Washabiki wa timu zote duniani tunajali mafanikio ya timu uwanjani...ambako tunapata furaha sana. Suala la mwekezaji kupata faida kubwa ni yeye sio sisi. Kama kweli sisi tunatska raha tuachane na mawazo ya kizamani ya uanachama mfu...mm kuwa mwanachama ilihali siwezi kufanya lolote timu yangu iwe bora kuliko nyingine that's useless!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijawahi kumwona mhindi akiendesha biashara yake Kwa hasara..... Simba ndo baibai... Nilikuwa nashangaa sana huu usajili hela inatoka wp? Ndo basi tena....Wanachama hamna sauti tena ndani ya club

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuwa na sauti wakati mfukoni huna kitu hizo ni kelele zenye karaha tuu.

Sent from my Compaq desktop-1997 Using Jamiiforums desktop app
 
Naunga mkono maneno yako Mkuu...... Mpira umebadilika zama hizi......mpira zama hizi ni pesa hao wazee wakiongozwa na mzee Kilomoni na Bi Hindu wanatia shs ngapi kuendeleza Club?
Timu haiwezi endelea kwa kutegemea gate collections na michango ya kununua kadi ya uanachama au ada ya uanachama.

Sent from my Compaq desktop-1997 Using Jamiiforums desktop app
 
Kwa nini Simba?Si ana pesa akaanzishe timu yake?
Kuna siku yatatokea maafa pale uwanjani,kwa sababu MO hawezi kukataa B5 ili simba ifungwe na yanga bao 6,itakuaje na timu tumempa bure?
Serikali iingilie kati suala hili ni bora awe Rais wa timu atumie nembo tu
 
Sahihi kabisa! Sisi mashabiki tunataka matokeo mazuri uwanjani tu! Hizo figusifigusi nyingine hazituusu.
 
hukumsikia siang'a!..ugomvi wake na mo mo alitaka zamalek wauziwe mechi,mkenya akadinda,matokeo yake akaenda kufundisha mtibwa
 
Ukweli ni kwamba Simba haipati chochote kwenye haya mauziano. Mo atatoa bilioni 20 ambazo zitaingizwa kwenye akaunti ya Simba kisha atakabidhiwa timu. Baada ya hapo yeye ndiye atakuwa na maamuzi ya mwisho kuhusu kila kitu ikiwa ni pamoja na matumizi ya hizo fedha. Atakuwa na hiari ya kubadili jina la timu au kuiuza na hakuna atakekuwa na mamlaka ya kuhoji. 'RIP' Simba Sc.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vita dhidi ya ufisadi ni ngumu sana, Simba wamebana weeeeeee mwisho wameachia!
 
Una akili sana!
 
Refer moses katumbi na Tp mazembe,Abrahamovic na Chelsea,Mimi naona sawa,hata kama hawatakua na sauti kumbuka tangu club ianzishwe,ilikuwa mikononi mwao kipindi chote hiko na hakuna cha maana walichokifanya,wampe Mo dewji naye aonyeshe uwezo wake.
Mo ni mpya pale Simba?!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…