Jeff Gemo
Member
- Jul 11, 2015
- 34
- 26
Habari wana JF na wapenda michezo!!
Hivi umewahi kujaribu kukinga maji kwenye tenga?? Au labda kutwanga maji kwenye kinu?? Haya ni matendo ya kishujaa sana yanayohitaji moyo wa ujasiri kuyafanya. Kama hukuwahi kuona basi tupo katika wakati muafaka, tutaona watu wenye ujasiri wakifanya matendo haya ya kishujaa.
Wapumbavu wana tafsiri nyingi sana, lakini tafsiri ninayoipenda ni ile iliyopo katika kitabu cha Mhubiri 7:9 "Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu". Mara nyingi nikiandika jambo wanakuja wapumbavu wengi sana, wanatukana na kwakweli mbarikiwe mno.
Mimi niliamua kuchukua kadi ya uanachama wa Simba Sports Club tarehe 23/07/1997 wakati huo Nikiwa mwajiriwa chuo cha ualimu Mpwapwa, Dodoma. Niliamua kuwa mwanachama ili nipate fursa ya kuhudhuria mikutano yenye kufanya maamuzi juu ya Club yetu.
Nalazimika kusema hivyo kutokana na watoto kunijia inbox na lugha chafu kana kwamba siifahamu hii club, watoto ambao hawajawahi kuiona katiba ya club yao, hawajui haki zao kikatiba zaidi ya kupiga kelele kama wendawazimu au vichaa, ni vijana wenye akili lakini hawana "manual" ya kutumia akili yao.
Mabadiliko ndani ya Simba yalianza muda mrefu sana, na tuliongea sana kushawishi sana kujiendesha kibiashara tangu wakati ule wa "Kidedea", tulifanya vikao halali na haramu kuhakikisha club inabadilishwa lakini haikuwezekana, hatukukata tamaa.
Safari hii hali tukampata MO, mtu ambae alikuwepo tangu wakati ule wa mwanzo kabisa, hatuna shaka juu ya mapenzi yake kwa Club, tukasema tutajitahidi tena safari angalau tupige hatua, yote hayo tuliyawaza kabla hawa vijana hawajui chochote kuhusu mabadiliko na hata tulipoyaleta waliyakataa na kuona Club imeingiliwa, hawa vijana walitukana sana na kusema hakuna kitu kama hicho.
Lakini kwa vile ni vijana wasio na uelewa wa jambo lolote, baadae wakakubali na kuanza kuyashangilia, wameyapokea na wanayataka haraka kuliko hata walioyatafuta, ni vijana wenye pupa wanaoweza kubadilika wakati wowote, vijana ambao wanatuoneasha hatuwezi kuwaamini katika kufanya maamuzi.
Wanachama wengi hawajui kabisa utaratibu wa kufuata kuyafikia mabadiliko wanayoyataka, wengi wamechoshwa na hali ya club kutokuwa na uwezo wa kuchukua vikombe kwa muda mrefu, wapo tayari kuibadili timu mradi wapate mafanikio ya kufurahisha nafsi zao, wanasema wao wanachoangalia ni ushindi tu na mengine hayawahusu.
Kama vijana wa zamani wangekuwa na mtazamo huo nadhani sasa hivi tusingekuwa na hii timu, hamuwezi kuwa wabinafsi kiasi hicho na kudhani ni ninyi peke yenu mwenye haki na hii timu, lazima mkumbuke mabadiliko ni kwa kizazi kilichopo na kizazi kijacho.
Hapa ndio tunafika kwenye suala la kuibadili katiba ili iweze kuilinda club yetu kwa vizazi vijavyo hata kama tutaiweka kwenye mikono isiyo salama. Ni katiba peke yake itakayotupa uhakika wa uhai wa Club yetu baada ya muwekezaji mwenye hisa nyingi kuondoka.
Lakini pia hatuwezi kurekebisha chochote kwa kumnufaisha mtu yeyote isipokuwa Simba Sports Club, maslahi juu ya Club yanapaswa kupewa kipaumbele na kuheshimiwa.
Kama ningepewa nafasi ya kutoa maoni ni kwa namna gani tunaweza kuibadili Club, nafasi ya ushirikishwaji washabiki wote ingekuwa kubwa kupitia njia mbalimbali kama mitandao, simu, fomu za maswali (questionnaires) na kadhalika, halafu baadae wanachama ndio wangepitia katika matawi yao na kukabidhi kwa wenyeviti wao ambao ndio wangekutana na kamati maalumu ya kufanikisha mchakato huu.
Sio suala la muda mfupi kwasababu matokeo yake ni ya muda mrefu, na pengine ni ya kudumu, huwezi kuyafanya kwa mikutano ya "ndio" na "hapana", ni kusababisha mitifuano na kesi zisizoisha Mahakamani, tutawatisha wawekezaji na hawatatamani tena kuja kwetu kwasababu wataona sisi ni wababaishaji.
Kwahiyo kwa mtazamo huo katiba halali ya Club ndio inaweza kufanya yote hayo, ni bora tuchelewe kuelekea mabadiliko lakini tumalize tofauti za ndani na turidhiane kwa sauti moja kama Wanasimba na ndipo tunaweza kupokea mapendekezo ya muwekezaji yeyote na yakapitiwa kuona kama yanakidhi viwango na akapewa nafasi. Hatutashindwa kama tutaenda kwa pamoja, kwa kufuata utaratibu maalum.
Mimi binafsi kama Jeff Gemo nimepata uzoefu mmoja kutoka kwa baadhi ya wanachama, ni watu wa pupa na hawawezi kufikiri kwa kutumia vichwa, walinitukana sana wakati wa mwanzo kabisa na hata kusema natumiwa kuiharibu timu, kwakuwa tu nilikuwa nadai mabadiliko. Watu hao hao waliotukana ndio leo wapo mstari wa mbele kuyataka mabadiliko na kuona tena kama mimi siyataki.
Simple logic, kama tulidai mabadiliko wakati tukiwa wachache, kwanini tuyakatae leo wakati tukiwa wengi? Je, hatukuwa na nia ya dhati ya mabadiliko hayo? Au hatujui ni nini tunataka? Hasha, tunaelewa nini tunataka, ni wapi tutakipata, vipi tutakipata na nani wa kutupa, kitu pekee tusichokifahamu ni wakati, yaani lini tutakipata.
Tunasimama kwa maslahi mapana ya Club, kwa faida ya kizazi cha leo na kesho. Haina maana ya kutafuta mabadiliko yatakayonufaisha kizazi hiki peke yake, Simba ina miaka 80 sasa na bado tunajivunia kama club yetu sote, na kila mtu ana haki na Club yake.
Ningependa nitoe Rai kwa wanachama, kabla ya kuyaendea hayo mnayodhani ni mabadiliko, ni vema mtafakari kwa kina tunapotoka na tuliyoyapitia, mtafakari nidhamu ya utendaji ya viongozi waliopo madarakani na mpime namna wanalivyopokea mabadiliko haya ambayo hawakutaka kuyasikia kabisa.
Mzitafute katiba zote mbili, ile ya mwaka 2010 na hii inayotumika ya mwaka 2014, mtu asiwaambie kila kitu kitakuwa sawa na kwamba msiwe na wasiwasi, jiridhisheni kwa kutembelea ofisi ya msajili wa vilabu mzungumze nao na kuelewa nini kinaendelea. Nendeni pia BMT mkaulize kama kuna shauri lolote lililowasilishwa na wanachama wa Simba kuhusu katiba ya Club, tafuteni Katiba halali na yenye baraka ndipo tunaweza kuendelea na jambo lolote lile.
Bado kuna siku kadhaa kabla ya tarehe iliyotajwa kuwa ni ya Mkutano mkuu wa dharura, twendeni tukiwa tunajua ni nini tunakwenda kukifanya na tunaelewa tukifanye vp! Siamini kama viongozi ndio wanatakiwa kutuelekeza sisi cha kufanya, nadhani sisi ndio tunatakiwa kuwaambia wao kitu cha kufanya kwasababu mamlaka tunayo na kama inawezekana basi tunaweza kutengua mamlaka yao na tukafuata utaratibu mwingine, muhimu katiba kwanza.
Lakini jambo muhimu la kujiuliza ni kwamba, agenda za mkutano ni zipi? Kwanini msipewe zote mzipitie mapema ili mjiandae kwa mjadala? Kwanini watu wawapeleke kama ng'ombe? Na kwavile wanajua wakitaja neno MABADILIKO mtakwenda na kumiminika kama Nyumbu, bila kuhoji jambo zaidi kwakuwa wamezisoma akili zenu na wanawaambia kile mnachotaka kusikia. Hakuna uwazi wala ushirikishwaji wa kikamilifu.
Lakini ikiwa wanafanya hivi kwa kumchezea akili "MO" na kuwahadaa wanachama hapo naweza kuelewa, na siwezi kuwalaumu kwasababu mnahesabu miezi iliyobaki mnatengeneza mazingira ya lazima kuonesha kuna jambo kubwa mnataka kulifanya kwahiyo mbakizwe madarakani.
Sina Imani na uongozi wa Aveva, lakini sina shaka na utendaji wao ikiwa tutakuwa pamoja kama timu, Aveva ni mzoefu, makamu wake nadhani ndio kiongozi pekee kati ya wote mwenye uzoefu mkubwa halafu "mjanja-mjanja" hivi, anaweza kutumia nafasi yake na uzoefu wake kutufikisha mbali, viongozi wa Simba wanaweza kufanya kazi nzuri sana ikiwa tutawasimamia badala ya "kuwasusia" kama tulivyofanya hapo kabla, na hatuwezi kusimamia viongozi ikiwa hatuijui katiba na hatujui mipaka ya viongozi kimaadili na kikatiba pia.
Nidhamu ni pamoja na kuheshimu katiba, kuifuata na kuilinda! kujiita Rais wakati katiba inasema kiongozi wa Club ni mwenyekiti, kuongoza Club comfortably kwa katiba "batili" takribani miaka miwili sasa na miezi kama mitano , uhalali wa kubadili katiba ambayo wala haikutambui unaupata wapi??
Mwisho kabisa nimuombe ndugu yetu Mohammed Dewji "MO" awe na moyo wa subra, tumedhamiria kufanya mabadiliko kwa misingi ya haki na kufuata muongozo wa katiba halali, hii itamsaidia yeye (Ikiwa atafanikiwa kupata 51% ya Hisa kama alivyopendekeza) kuendesha timu kwa amani, umoja, upendo na ushirikiano.
Mohamed Dewji asingepeta kuonekana kama amevamia Club na kutumia nguvu ya pesa kupata kuwekeza pale, ni mfanyabiashara mwenye heshima kubwa Afrika na Dunia nzima, ni mtu aliye mstari wa mbele kutetea wanyonge na kusaidia wasiojiweza, naweza kusema "MO" ni tajiri mwenye utu, na asiyetumia pesa kama fimbo, tangu akiwa mbunge mpaka anaondoka ametuonesha ni mtu anayejali sana wananchi.
Ni picha mbaya ikiwa MO atachukua timu huku malalamiko na kelele za wenye timu zikimuandama, ni sifa mbaya kwake na itamchafua kwa watu wengi wanaomuamini na kuunga mkono juhudi zake katika jamii, ninaamini hawezi kukubali na hayupo tayari kuchafua jina lake.
Serikali yetu ipo na haijalala, ni serikali inayoongozwa kwa utawala wa sheria, ninaamini itakapolazimika basi itaingilia kati na haki itatendeka, na itawalinda wawekezaji wetu kwa misingi ya sheria, na kuhakikisha amani inatamalaki ndani ya Club yetu.
Niwashukuru wote watakaoamua kuchukua hatua kuyaendea mabadiliko ya kweli, mabadiliko ya club kwa faida ya sasa na baadae, mabadiliko halali yenye kujawa na amani, upendo, umoja na ushirikiano.
Simba Sports Club - NGUVU MOJA
Jeff Gemo Mnyama Machine
The One Man Army
Affirmative Gemo The Great
[HASHTAG]#SeriesFreeLife[/HASHTAG]
Release date: 22/11/2016
Release time: +0350 (GMT)
PGA