Zanzibar 2020 Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF) umempitisha Mussa Haji Kombo kuwa mgombea wa Urais Zanzibar kwa tiketi ya CUF

CUF Habari

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2019
Posts
239
Reaction score
234

MKUTANO MKUU WA TAIFA WA CUF CHAMA CHA WANANCHI UMEMPITISHA MUSSA HAJI KOMBO KUWA MGOMBEA WA URAIS ZANZIBAR KWA TIKETI YA CUF

Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Wananchi (CUF) umempitisha Mussa Haji Kombo kuwa Mgombea wa Urais visiwani Zanzibar kwa asilimia 66 ya kura zote.

Wagombea wengine katika mchakato huo walikuwa Eng. Mohamed Habib Mnyaa aliyepata asilimia 19 za kura na Rajab Mbarouk Mohamed aliyepata asilimia 15.

Kwa upande wa Tanzania, CUF imepitisha Prof. Ibrahim Lipumba ambaye aliungwa mkono na asilimia 97% wa Wajumbe.
 
Cuf ipi hiyo unaizungumzia hapa?
Kwa ujinga wenu wenyewe mlisha ihujumu cuf yenye heshima na sifa ya kuwa chama cha upinzani.

Kwa tamaa zenu na Lipumba mlikubali kuiuza cuf sasa imebakia na jengo tu na bendera tu. Mwaka huu nawahakikishia kuwa hata diwani mmoja hamto mpata.

Hiyo ndiyo dawa ya wasaliti popote duniani.
 
nyinyi mliyo mpitisha lowasa kisha mkawaminisha watu kuwa huyu ni msafi ilihali mlikwisha sema ni fisadi ndio wapinzan wa kweli ama kweli nyan haon kundule
 
Cuf mlisha iuza kwa ccm kitambo na mfaidika mkuu ni Lipumba
nyinyi mliyo mpitisha lowasa kisha mkawaminisha watu kuwa huyu ni msafi ilihali mlikwisha sema ni fisadi ndio wapinzan wa kweli ama kweli nyan haon kundule
 
Cuf ilisha jimaliza yenyewe kwa kukubali kumrudisha kundini Lipumba
Chagueni hvi leo mutakae mtumikia, kama ni ccm basi ungeni mkono juhudi mazima, la hasha kama ni wananchi basi tumikieni wananchi na muache kutanguliza tumbo mbele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…