Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Polisi walivamia ofisi za CHADEMA mapema leo asubuhi na kuzuia mkutano huo kufanyika wakisema wataleta usumbufu wakati mkutano wa nishati unaendelea, na kwamba wanatakiwa kughairisha.
Mkutano ambao ungekuwa na waandishi wa habari tu kurusha tukio hilo, tena mbali kabisa na Posta ambako wageni hao wanapokelewa na mkutano kufanyika.
Wakati huo huo chawa wamefanya event pale feri karibu kabisa na Ikulu, wamekata keki ya mama na kugawa mitungi ya gesi kwa hapo feri!
Soma Pia: Jeshi la Polisi lazingira Ofisi ya Makao Makuu CHADEMA Mikocheni na kuzuia Mkutano wa Mnyika na Waandishi wa Habari
Wao na CHADEMA nani angeweza kuleta vurugu kwenye mkutano huo?
Serikali/CCM imeogopa lingetoka tamko la kuwachoma wakaaibika mbele ya wageni wa kimataifa? Au waliogopa kufunikwa na mkutano wa CHADEMA?
Hii move inatoa ujumbe gani Wakuu?