Mkutano wa Dharura wa Utatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi hiyo uliofanyika kwa njia ya mtandao katika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 5

Mkutano wa Dharura wa Utatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi hiyo uliofanyika kwa njia ya mtandao katika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 5

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC- Organ), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Mkutano wa Dharura wa Utatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi hiyo uliofanyika kwa njia ya mtandao katika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 5 Januari, 2025.

Viongozi wengine walioshiriki katika mkutano huo ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Stergomena Tax ( Mb.), Katibu Mkufu Wizara ya Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi, Dkt. Samwel Shelukindo na Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe.

Mkutano huo pia umehudhuriwa na Nchi za Zambia na Malawi ambao ni wajumbe wa Utatu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (Organ Troika).

Pamoja na masuala mengine mkutano huo umejadili na kutoa mapendekezo ya namna SADC inavyoweza kuisaidia Jamhuri ya Msumbiji kukabiliana na changamoto za kisiasa zinazoendelea nchini humo.

Msumbiji imekumbwa na machafuko ya kisiasa kufuatia chama cha upinzani kutokubaliana na matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika tarehe 09 Oktoba, 2024.
 
Attachments

  • FB_IMG_1736106918604.jpg
    FB_IMG_1736106918604.jpg
    45.8 KB · Views: 4
  • FB_IMG_1736106934494.jpg
    FB_IMG_1736106934494.jpg
    58.2 KB · Views: 4
  • FB_IMG_1736106930200.jpg
    FB_IMG_1736106930200.jpg
    87.3 KB · Views: 3
  • FB_IMG_1736106938960.jpg
    FB_IMG_1736106938960.jpg
    90.3 KB · Views: 4
  • FB_IMG_1736106936959.jpg
    FB_IMG_1736106936959.jpg
    83.4 KB · Views: 4
  • FB_IMG_1736106925526.jpg
    FB_IMG_1736106925526.jpg
    49 KB · Views: 3
  • FB_IMG_1736106922595.jpg
    FB_IMG_1736106922595.jpg
    64.9 KB · Views: 2
  • FB_IMG_1736106920650.jpg
    FB_IMG_1736106920650.jpg
    102.7 KB · Views: 4
  • FB_IMG_1736106927538.jpg
    FB_IMG_1736106927538.jpg
    73.9 KB · Views: 5
  • FB_IMG_1736106932051.jpg
    FB_IMG_1736106932051.jpg
    42 KB · Views: 2
Yeye Rais Samia ndiye anaongoza hii Trinity ya Siasa,Ulinzi na Usalama, lakini vurugu zimeendelea kule Msumbiji hakuna chochote kilichofanyika na Tanzania.
Tumeona Anthony Blinken alivyokuwa anakwenda Tel Aviv tena na tena baada ya hii vita kuanza na Hamas.
(Na huyu Anthony Blinken amekuwa very quiet siku hizi. I wonder why. Lavrov is taking the world by storm)
Sasa nasikia watu wanaongea kuhusu kuwaleta wale , Mondlane,na huyu mwingine sijui anaitwa nani,( nisije nikakosea jina nikaanzisha vita)kwenye meza ya mazungumzo.
Nadhani diplomats wenyewe wanajua jinsi wanavyotanzua haya matatizo.
Lakini inasikitisha kwamba tulivyokuwa tunayatazama haya matukio ya Msumbiji tulikuwa tumesahau kwamba yanatuhusu kama nchi inayoongoza hiyo Trinity.
Siyo tu chaos Msumbiji lakini pia tunasikia minong'ono imeanza tena huko Ziwa Nyasa wakati kulikuwa shwari Rais Samia alipoingia madarakani.
Nakumbuka yule the Great Man, Sheikh Thabit Kombo.
Lakini huyu Thabit Kombo jr. I wonder if he is being sluggish.
 
Political issues they have never been a solution to social problems
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC- Organ), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Mkutano wa Dharura wa Utatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi hiyo uliofanyika kwa njia ya mtandao katika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 5 Januari, 2025.

Viongozi wengine walioshiriki katika mkutano huo ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Stergomena Tax ( Mb.), Katibu Mkufu Wizara ya Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi, Dkt. Samwel Shelukindo na Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe.

Mkutano huo pia umehudhuriwa na Nchi za Zambia na Malawi ambao ni wajumbe wa Utatu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (Organ Troika).

Pamoja na masuala mengine mkutano huo umejadili na kutoa mapendekezo ya namna SADC inavyoweza kuisaidia Jamhuri ya Msumbiji kukabiliana na changamoto za kisiasa zinazoendelea nchini humo.

Msumbiji imekumbwa na machafuko ya kisiasa kufuatia chama cha upinzani kutokubaliana na matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika tarehe 09 Oktoba, 2024.
HUYU Mkuu wa nchi Kuna Nini???

Mbona anakimbia daima Ikulu ya Dodoma 🦤 na Magogoni?? Au ndio jogoo kawika 🦤🦤🦤🦤🤣🤣🤣🤣🤣Nyangaaaa gweeeer🤣🤣🤣🤣🤣🤸🤸
 
Huyu mtu angekua anajielewa angepumzika tu.
 
Back
Top Bottom