Elections 2010 Mkutano Wa Hadhara Wa Wana-JF [Online]


Du! Recta ulikuwa wapi muda wote huu toka jana?

Kwa kweli nondo zako ni makini sana na zimekamilika.

Hata hivyo ukipenda kuboresha zaidi unakaribishwa.

Hii issue ya Ulinzi na Usalama, unaweza ukaielezea kwa undani zaidi?
 

HGoja yako ya 1 na ya 4 ziko vizuri. Hili la 2 na la 3 ni very interesting.

Unaweza ukalitolea ufafanuzi wa kina ili wadau walielewe vema?
 

Mwenyekiti Mwenza, hebu pitia hoja hizi uone kama hajatukana huyu mangi . . . haaa haaa
 
Teh teh teh! Akirudi Superman hapa utamueleza kwa nini umefanya mabadiliko! Kwani amekuachia full madaraka?

Balozi, naomba tu nukubali maana huyu DC alikubali, halafu akakataa kisha akaingia mitini. Mimi naona tunendelee tu na wewe unafanya kazi njema pia.

Asante san Msanii kwa uongozi makini.
 
Mwenyekiti kaingia mitini bila kuahirisha kikao wala kumuachia kaimu nini? Nasikia harufu ya futari, baadae kidogo.

jamani Msanii kaingia mitini naye? Ndo maana nimekuta fujo sana niliporudi.

Anyway katibu, pole na kazi nzito sasa tuendelee.
 
Ok nimepata taarifa toka kwa mwenyekiti wa dharura kuwa amepatwa na dharura hivyo atakuja kwa dharura baada ya kumaliza dharura. Ni majibu ya dharura baada ya dharura hii.

Mangi . . . Mangi . . . Vijana wa Kova wako hapa. Usinichakache mimi.
 

Mkuu, hoja zako ni nzuri sana. Ila tuepuke kutaja vyama maana huu ni mkutano wa Kitaifa zaidi.

Hoja zako ni za nguvu na tutaziweka kwenye majumuisho.
 

Baba lao hoja zako No. 2 hadi 5 zinakubalika na umeziuongelea vizuri sana. tayari ziko kwenye mchakato wa majumuisho.

Hili la kwana linavutia sana na kuna ubunifu zaidi. unaweza ukalitolea ufafanuzi wa kina?
 

Hili la Ukomo kwa wabunge nadhani ni hoja nzuri sana. Hebu iweke vuzuri kwa undani wadau waifahamu.

Hili la sitting allowance WoS alishalitolea ufafanuzi.


Mkuu, ungesubiri mkutano uishe basi ndo uendelee na Vi-cans vyako. ama?
 

.
Nimekupa mheshimiwi m/kiti. Uchakachuaji wa mapenzi tunaweza tukauthibiti ikiwa ya kwamba dhamira zetu kama taifa zitasukumwa na nia ya dhati ya kusimamia maadili na utamaduni wa mwafrika.
Haya tutayafanya je? Ni lazima tutenganishe dini na serikali. Na kufanikisha hili napendekeza kuwepo na baraza linalowahusisha wakuu wote wa kidini ili waweze kutoa ufafanuzi kwa vyombo vya kisheria vya serikali pale itakapotokea mtafaruku wa mapenzi na mahusiano kwa hizi jinsia mbili. Kuna wanaoruhusika kuwa na mke mmoja, na pia kuna wanaoruhusika kuwa na mke zaidi ya mmoja na hii ni kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizo ndani ya dini zao. Hakuna kitabu chochote cha dini yoyote ya Mungu wa kweli, kinachosema mke aweza kuwa wa jinsia moja ni mme.
Mkuu wa meza nawakilisha.
 

.
Aaah bana, nchi hii kuna linaloshindikana? Mmenikabizi kwa Kova, tukiwa njiani kuelekea kituoni ilinilazimu kuongea kwa herufi kubwa. Ameniachia na ndio maana mnaniona hapa mkutanoni.
Japo nimeonywa kubadilika, lakini ni nani aliye ndani ya moyo wangu ajue kama nimebadili msimamo? M/kiti utanikabizi MIC mara moja tena kabla ya mkutano kufungwa?
 
Elimu, afya, kilimo ni std. & general agenda ambazo zinaimbwa kama vibwagizo kila mwaka wa uchaguzi.

Nadhani tunahitaji more pragmatic agenda ambazo tunaweza kuona matokeo baada ya miaka mitano kama vile:
  • Kuboresha mji wa Dar (Dar ndiyo ''reception hall'' ya TZ). Ni chafu, hamna maji, haina mpangilio, misongamano, n.k.
  • Kutokomeza malaria TZ (manageable)
  • Constitution inayoeleweka (piece of cake kukiwa na utashi ..) na agenda zingine specific na zinazotekelezeka kama hizi
 
Mkuu umeiboresha vyema sana hii kitu. Naunga mkono kuwa hoja kuhusu UwT ni kuitazama sheria inayoiunda kisha kutafakari kwa kina namna ya kuifanya iwe bora zaidi kwa taifa hili. Hivyo serikali itakayoingia madarakani inapaswa kufahamu kwamba UZALENDO si kuwalinda viongozi bali kulitumikia TAIFA na kulifia TAIFA.
Thanx mwenyekiti umerudi
 

Kiby hii issue uliyoianzisha ni nzito saaana. Imejikita katika sehemu tatu: Haki Za Binadamu; Maadili Na Dini.

Labda bila kwenda ndani sana linaweza likaingizwa katika katiba likiwa chini ya haki za binadamu "Kwamba Kila Mtu ana Haki ya Kupenda na Kupenda"

Sijui unaonaje?
 


Kijana wangu usiniambie kuwa umetoa rushwa na Kova kapokea? Hilo ni kosa kwa mujibu wa sheria.

Tutafika kweli? Tufanyeje ili kumaliza tatizo hili la Rushwa iliyokithiri?


Haya Kamata Mic umalizie hoja zako.
 

Mkuu Cynic unajua agenda ulizozitaja ni kali sana na mpaka sasa hakuna aliyezitaja:

Unaweza ukazielezea kwa undani ili Wana-JF waweze kulielewa vema?

Hongera sana. Please kamata Mic.
 

kamnanda Tuko pamoja.

Unajua nafasi ya UwT katika uendeshaji wa Serikali na kusimamia Maslahi ya Nchi ni kubwa sana. Ni vema wasijihusishe na siasa kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…