Balozi, naomba tu nukubali maana huyu DC alikubali, halafu akakataa kisha akaingia mitini. Mimi naona tunendelee tu na wewe unafanya kazi njema pia.
Asante san Msanii kwa uongozi makini.
Du! Recta ulikuwa wapi muda wote huu toka jana?
Kwa kweli nondo zako ni makini sana na zimekamilika.
Hata hivyo ukipenda kuboresha zaidi unakaribishwa.
Hii issue ya Ulinzi na Usalama, unaweza ukaielezea kwa undani zaidi?
Kwa hapo M/Kiti naona unataka kuharibu kikao. Naomba uthibitisho wa hilo kabala sijaomba msaada from somewhere! Usipoangalia tutalazimika kurudia yale mambo ya Freedom square na Nkurumah kabla hujafunga kikao!!
Kuna DC mwingine unayemzungumzia au Dark City?? Kama ni huyo nadhani hujasoma vizuri posts zake. Kazi njema na Lunch njema pia.
Nashukuru Mwenyekiti (Superman) kwa comments zako kuhusiana na mchango wangu wa mawazo katika thread hii.
Ni bahati mbaya kuwa nilichelewa kuona kikao kikiendelea. Japokuwa nilikuwa nimechelewa sana, sikuona kulikuwa na ubaya wowote kuchangia hasa kwa kuwa deadline haikuwa imefika.
Yes, kwa hakika ninaweza kabisa kuiendeleza zaidi hoja ya ulinzi na usalama. Naweza kufanya hivyo kama ifuatavyo.
Katika kuimarisha ulinzi na usalama wa Taifa, serikali ijayo inatakiwa kuzingatia yafuatayo:
Ulinzi na Usalama unaokidhi mahitaji, una uwezo mkubwa wa kujenga na kuimarisha uzalendo. Nchi yenye amani ina kila sababu ya kupiga hatua za maendeleo kwa haraka na wananchi wake kuweza kujivunia utaifa wao. Ili kujenga uzalendo huo, wananchi wanatakiwa wawe na imani na vyombo vyao vya ulinzi na usalama na uahkika wa usalama wa mali zao na familia zao kila wakati.
- Kuunganisha Wizara ya Mambo ya Ndani na Ulinzi kuwa wizara moja inayoweza kuitwa Wizara ya Ulinzi na Usalama na Mambo ya Ndani. Hii itasaidia kuweka mikakati ya pamoja katika majeshi yetu na kushirikiana kila inapohitajika katika kuhakikisha kuwa nchi inakuwa salama wakati wote.
- Kuimarisha vyombo vyote vya ulinzi na usalama kwa kuviwezesha kwa kuvipatia zana za kisasa, mafunzo/utaalamu na kuondoa watumishi wasio na wito, nidhamu na wanaovunja sheria za ajira zao na mategemeo ya nchi. Hii itachangiwa pia na ongezeko la bajeti ya ulinzi na usalama
- Kuhakikisha kuwa uhamiaji haramu (hasa katika maeneo ya mipakani ya nchi) unadhibitiwa. Hii itapunguza matukio ya ujambazi katika mikoa ya jirani na mipaka hiyo, na vile vile kupunguza urahisi wa majambazi kutorokea nchi jirani kila wanapokamilisha matendo ya ujambazi na uvunjaji mwingine wa sheria.
- Kuhakikisha kuwa waTanzania wote wanatambulika (kuwa na vitambulisho vya Taifa)
- Kushirikisha zaidi wananchi katika masuala yote ya ulinzi na usalama. Wananchi wanatakiwa kutoa taarifa zozote zinazoweza kusaidia vyombo vya ulinzi na usalama kubaini na kuzuia makosa ya jinai na hasa ujambazi, udhalilishaji wa watoto, mauaji n.k. Utaratibu mzuri zaidi wa kuhakikisha wananchi wanalindwa kila wanapotoa taarifa za kusaidia kufichua waovu.
- Kuhakikisha kuwa, wanajeshi na Polisi wote wanaishi katika kambi ili kuwahakikishia usalama wao na wa familia zao. Lakini vile vile, kuwafanya wasiweze kurubuniwa kwa urahisi na watu wenye nia mbaya ya kuwapotosha katika utendaji wao wa kazi
- Kuhakikisha kuwa askari wote wanapata mishahara mizuri na mafao mengine kwa wakati na ukamilifu ili kuwapunguzia tamaa ya kushiriki katika vitendo vya uvunjaji wa sheria
- Kupunguza ukubwa wa jeshi la Wananchi na kuongeza ukubwa wa jeshi la Polisi. Hii ni kwakuwa, ukanda mzima wa Afrika mashariki hauna matukio makubwa ya vita na kwa jeshi la wananchi kuwa idle kwa muda mrefu, kunawafanya wapate hamasa ya kufanya vitendo viovu kwa jamii. Vile vile, hakuna sababu ya kuwa na jeshi kubwa lisilo na kazi, wakati jeshi la Polisi likiwa na upungufu wa human resources.
Naona wikend inasababisha dharura iwe kawaida sasa.
Enewei bado changamoto hewani maana kila tunapoikabili siku mpya mambo huwa bado kabisa. I mean tumesimama badala ya kutembea kiuchumi.
Hili nalo NENO
Naona tuna wazalendo wachache wakiongozwa na KATUBU wanataka kuongea hapa. KAribu uanze Ambassador kisha tuendelee wengine.
Ambassador
Kitongoli
Mujuni2
Jungumawe
Mwenyekiti ameenda kutabaruku kidogo, mimi makamu wake nakukaribisha utoe dukuduku lako la maoni.Nasubiri zamu yangu mwenyekiti lol!
Katibu wetu Ambassador hajalala tokea juzi akiwasubiri nyooote mtoe michango yenu kisha afanye majumuisho ya pamoja.Mwenyekiti, tumeongelea mambo mengi sana. Nasikitika katibu wa kikao anasinzia sinzia (sijui na yeye anasumbuliwa na ule ugonjwa)?? Nashauri atafutwe katibu wa dharura aandae summary ya mambo yaliyojadiliwa maana raisi wetu (Mtarajiwa) ameniomba tumpelekee minutes za kikao hiki muhimu
Mkuu Mkandara ondoa shaka, itifaki imezingatiwa na hoja zote humu ni muhimu na zinafanyiwa majumuisho ili kuepuka kurudia rudia hoja na pia DIRA hii itawasilishwa kwa rais atakayeapishwa ili ajue pamoja na sera za chama lakini kuna mambo nyeti ya kuzingatia ambayoNINYI WOOTE Mmechangia uhuishaji wakeWankuu zangu,
Mengi yamezungumzwa na yote ni muhimu sana kwa mapana yake. yaani vichwa vipo JF isipokuwa moja tu naloomba mliwekee maanani kwa sababu haya myatakayo ndiyo yanaunda DIRA ya TAIFA (TANZANIA DEVELOPMENT VISION). Sasa sielewi kama mwenyekiti na wasaidizi wako mumeweza kuyapanga yoote kwa kadri jinsi wanabodi wanavyochangia ili kupata kitu kimoja saafi.
Sina zaidi isipokuwa kutoa shukran zangu kwa wachangiaji ambao hakika wamegusia kila sehemu ipaswavyo. Tahadhali ni moja tu kwamba hatuwezi kwenda mbele pasipo kurekebisha kile kilichotukwamisha...Na nyote mnakijua vizuri..
Mkuu, hizo ni idara tisa tu ambazo kwa kiasi kikubwa zinasimamiwa na nidhamu za kijeshi zaidi ya utawala wa kisiasa. Naamini kabisa kuwa, zinaweza kuwa chini ya wizara moja na zikawa na ufanisi mkubwa kuliko ilivyo sasa.Du! Recta kijana wangu, unatisha, sikuwahihi kulifikiria hili la kuunganisha Wizara; Masuala ya Ulinzi na Usalama(Mipaka na Washika bunduki yako katika idara sifuatazo:
Je, hivi vyombo vyote vinaweza kushughulikiwa na Wizara moja?
- TPDF
- JKT
- Police
- Magereza
- Uhamiaji
- Wakimbizi
- Zimamoto
- Usalama Wa Taifa
- PCCB
kumbe ni porojo tu za kusogeza muda mbele ndicho kinachoendelea hapa....:becky:
Mkuu NNkumbe ni porojo tu za kusogeza muda mbele ndicho kinachoendelea hapa....:becky: