naona nikuite mwenyekiti, ni sawa kabisa, nina uchungu sana na hawa mafisadi,la sivyo nitajichukulia hatua mkononi ya kuwachoma bisibisi za kichwani kama hawataadhibiwa
Mie yakhe napendekeza katika uundaji wa katiba mpya kuwe na kifungu cha sheria kinachomlazimisha yeyote ataekabithiwa madaraka ya usimamizi wa rasilimali za nchi, kula kiapo cha ikiwa atahujumu uchumi wa nchi na ikathibitika kisheria, basi akubali kwamba atanyongwa hadharani. Hii itapunguza msongamano wa watu wanaotafuta madaraka kwa gharama isiyomithilika. Kuna mifano iliyo hai wapo wanaoitafuta ofisi kwa kuteketeza bil 50. M/KITI NASISITIZA TENA LAZIMA WATU HAWA WALE KIAPO HIKI CHA KUNYONGWA HADHARANI IKIWA........
M/kiti, pointi ovu interapusheni! nilipitwa..
1. Tunahitaji viongozi waadilifu (credible) na wawajibikaji (accountable) wawe mfano kwa taifa la leo na vizazi vijavyo.
2. Tunahitaji kuandika katiba mpya kabisaa!
Asante sana Kijana wetu Kiby,
Hakika unaonyesha una uchungu sana na Nchi hii ya Maziwa na Asali . . . .
Kwa hiyo unachosema ni kuwa "Kiongozi Wa Kuchaguliwa Atakayepatikana Anahujumu au Kuifisadisha Mali ya Taifa, Anyongwe Hadharani Mpaka Afe"?
Sasa hapa pana mgogoro kidogo? hatutakuwa tumevunja haki za binadamu? Wanaharakati mnasemaje kwa hili?
Kuna mfano wowote wa Nchi wanaofanya hivi?
Naungana na wadau hapo juu Mwenyekiti, tunahitaji Katiba na Kiongozi atakayerudisha nchi na watu wake kwenye mstari! Mambo mengine yatajipa tu!
Tunahitaji mtu atakayefuata rule of law, utawala bora, atakayeimarisha Muungano kwa kuirudisha Tanganyika na cha msingi zaidi tuwe na katiba mpya.
Kuna mahali nilisoma Slaa akipata ridhaaa ataweka katiba mpya ndani ya miaka michache ya uongozi wake! Jamani hebu nipeni info zaidi .....jirani zetu imewachukua zaidi ya miaka ishirinini (Kenya) hadi walipoiwekea sahihi juzi....
Jamaa kapotea na bahasha zetu za khaki!!!!!tunataka mgawo wetu haiwezekani.
Mwenyekiti, napendekeza iundwe " task force" itembelee nchi kadhaa kujifunza uzoefu wa namna sheria kama hii inavyofanya kazi...tukianza na China.....( mhhh...sijui itatumia mabilioni mangapi!)
You people can think. Thanx!
M/kiti..hoja yangu ya kupata uzoefu nchi nyingine umeipuuza?
Kiongozi Genakai, nilikutafuta sana tulipoanza sikukuona? Vipi mbona umechelewa kwenye mkutano? majukwaa yote sikukuona ama ulikuwa "kwenye lile lingine"
Kwa heshima na taadhima naomba sasa nikukaribishe utoe maoni yako.
WoS asante sana . . . Wana JF naomba tushauriane . . . tunahitaji kweli Task Force ili kujua agenda kuu 2010 ambazo tunataka zifanyiwe kazi?
Mimi naomba kwa kuwa hizi ni zama za utandawazi, basi pitieni katika wavuti na tovuti mbalimbali ili kupata facts. Hii itasaidia kuokoa mamilioni mabyo yangesaidia maendeleo ya nchi yetu kama kujenga shule na dispensary nk.
Sijui Wos na wengine mnalionaje hili? Kama tuko pamoja basi tupate data ya mifano ya huko China ni nini kinaendelea kabla hatujakubaliana.
Si unajua mambo ya chuo, nilikuwa busy kudogo na my theses supervisor ananielekeza. But hakijaharibika kitu. Kimsingi nadhani hao jamaa watakao ingia basi wawe na uchungu na nchi kwelikweli na hii hali ya ubinafsi jamani tuiache ili yuwe na mtazamo wa maendeleo ya nchi kwa ujumla!