Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Mkutano wa kutathmini hali ya Siasa hapa nchini uliandaliwa na REDET katika ukumbi wa Mkrumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam umemalizika rasmi na haya ndio mapendekezo ya mkutano huo.
Mkutano huo ulikuwa ufunguliwa na rais Jakaya Kikwete, lakini kutokana na hali yake (uchovu), amemtuma waziri Mkuchika kuufungua.
Katika hotuba ya rais, kama kawaida imejaa habari njema nyingi za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM kana kwamba hiyo ndio hali ya siasa ilivyo hapa nchini kwa sasa.
Hata hivyo, hotuba hiyo, haikuzungumza lolote kuhusu hali ya sasa ya Pemba, wala hakuzungumzia tena prospects za muafaka, ama maendeleo yoyote ya kisiasa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, au maandalizi ya uchaguzi Mkuu ujao.
Pia REDET imezindua kitabu kinachochambua kwa kina mustakabali wa Dini na Siasa za Tanzania.
Mkutano umehudhuriwa na wanasiasa, viongozi wa dini, wanaharakati, wanabalozi wanaoziwakilisha nchini zao humu nchini, wahadhiri, wanafunzi na wananchi wa kawaida.
Leo ninamalizia kwa kuwaletea majumuisho haya katika hii attachment.

Attachments
Last edited by a moderator: