Mimi niliiona mkutano wa Arusha kwa luninga nikiwa Morogoro kupitia Star TV siku ya Ijumaa na Jumamosi. Bahati mbaya sauti haikutoka vizuri na haswa Jumamosi sauti haikusikika kabisa. Watu wengine niliongea nao wakiwa Dar walisema walikuwa wanasikia vizuri, sasa sijui kwa nini Morogoro sikuweza kupata sauti. Niliporudi Dar Jumapili tarehe 7 ndio ilikuwa siku ya mwisho, nilimsikia vizuri sana kupitia Star TV. Ujumbe mmoja wapo muhimu nilioupata ni kwamba kufanya dhambi huondoa uwepo wa Mwenyezi Mungu, hivyo tujitahidi kufanya maombi ya toba ili kuongeza uwepo wa utukufu wa BWANA.