Elections 2010 Mkutano wa Kampeni wa Rais Kikwete Mbinga katika Picha
Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Jakaya Kikwete, akipungia wananchi waliofika uwanja wa ndege wa Mbinga mkoani Ruvuma kumuaga mara baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni jimboni humo Oktoba 11, 2010
Wananchi wa Mbinga wakishangilia msafara wa Mheshimiwa Kikwete
Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Kikwete akicheza ngoma ya chihoda iliyokuwa ikichezwa na akinamama wa kabila la wamatengo wa mjini Mbinga muda mfupi kabla ya kuhutubia mkutano mkubwa wa kampeni
Mgombea Urais kupitia CCM Mheshimiwa Jakaya Kikwete akiangalia ngoma ya mganda huko mjini Mbinga kabla ya kuhutubia mamia ya wakazi wa mji huo katika siku yake ya pili ya kampeni katika mkoa wa Ruvuma

Rais Jakaya Kikwete ambaye ni mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi akisalimiana na wananchi mbalimbali wa mji wa Mbinga waliojawa na shauku kubwa ya kuonana naye kabla ya kuhutubia mkutano mkubwa wa kampeni.

Mganda
Umati wa wana Mbinga wakimsikiliza Mheshimiwa Kikwete ambaye ni mgombea wa urais kupitia CCM akihutubia mkutano wa kampeni
Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Jakaya Kikwete, akiungana na wasanii wa ngoma za asili wilayani Mbinga mkoani Ruvuma, kucheza ngoma ya Lizombe.
Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Jakaya Kikwete, akiungana na wasanii wa ngoma za asili wilayani Mbinga mkoani Ruvuma, kucheza ngoma ya Lizombe.
Wasanii wa ngoma za asili mkoani Ruvuma wakitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni uliohutubiwa na mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Jakaya Kikwete, Oktoba 11, 2010
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mtoto mlemavu Maria Chiwinga muda mfupi baada ya kuwasili mjini Mbinga jana ambapo aliwahitubia wananchi katika mkutano mkubwa wa kampeni.Dr.Kikwete aliahidi kumpatia mlemavu huyo msaada ili aweze kuendelea vyema na masomo yake.
Mheshimiwa Kikwete akiweka ishara ya ushindi kwa wana CCM wa Mbinga waliojitokeza kwa wingi kusikiliza mkutano wa kampeni mkoani Ruvuma.
source. jakayakikwete.blogspot.com
source. jakayakikwete.blogspot.com
Ngoja nayo niichunguze kama ipo hosted kule 6telecoms